>
POLITICS
>
.UVCCM WAMALIZA KIKAO CHA BARAZA
.UVCCM WAMALIZA KIKAO CHA BARAZA
Posted on
Sep 13, 2012
|
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Ndugu Martine Shigela akichangia ajenda katika kikao cha Baraza la Umoja huo,(katikati) ni Makamu Mwenyekiti Ndugu Beno Malisa na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Mfaume kizigo, wakiwa katika kikao cha Baraza hilo kililofanyika Jana tarehe 12 katika ukumbi wa sekretarieti maarufu kama (white house) uliopo Makao Makuu ya Chama, Dodoma.
Baadhi ya maafisa na watendaji wa Umoja wa Vijana,Wa kwanza kushoto Ndugu Shara Ahmed (Mkuu wa Kitengo Cha Oganaizesheni Unguja) Ndugu John Melele (Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uchumi) Ndugu Deogratius Daffi (Mhasibu Mkuu) na Ndugu Salmin Dauda(mwenye laptop) Mkuu wa Kitengo Cha Benki ya Vijana)
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji Taifa UVCCM,ambae pia ni mjumbe kikao Cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Ridhwan J. Kikwete akichangia hoja katika kikao Cha Baraza hilo kilichofanyika jana, tarehe 12, Makao Makuu ya Chama,Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)
Mjumbe wa Baraza la vijana (UVCCM) ambae pia ni Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mheshimiwa Abdalah Ulega akichangia jambo katika Kikao hicho kilichofanyika jana katika ukumbi wa Sekretarieti, Dodoma.
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wakifuatilia hoja kutoka kwa mmoja miongoni mwa wajumbe katika mjadala wa kupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Umoja huo ngazi ya Mkoa na Taifa.