photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > ALI ZEIDAN AUKWAA UWAZIRI MKUU NCHINI LIBYA.

ALI ZEIDAN AUKWAA UWAZIRI MKUU NCHINI LIBYA.

Posted on Oct 15, 2012 | No Comments

Mwanadiplomasia wa zamani wa Libya Ali Zeidan (Pichani) amechaguliwa na Bunge la nchini hiyo kuwa Waziri Mkuu mpya pamoja na kuwa anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuliteuwa baraza la mawaziri, ambalo litakubaliwa na vyama vyote katika nchi hiyo.
Mtangulizi wake, Mustafa Abushagur ameondolewa baada ya kura ya kutokuwa na imani naye bungeni mwanzoni mwa mwezi huu, baada ya mawaziri aliowateua kupingwa ndani na nje ya bunge hilo.
Libya inahitaji haraka serikali ili kuweza kuikarabati nchi iliyoharibiwa na vita na kuleta maridhiano miongoni mwa raia baada ya mgawanyiko uliosababishwa na vita vya kumuondoa madarakani Kanali Muamar Gaddafi.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru