BINTI MWANAHARAKATI WA PAKISTAN ALIYEPIGWA RISASI KICHWANI AWASILI UINGEREZA KWA MATIBABU.
Posted on
Oct 16, 2012
|
No Comments

Malala Yusoufzai.
Msichana
wa Kipakistani aliyepigwa risasi kichwani wiki iliyopita kwa sababu ya
kampeni yake kwa elimu ya wasichana Malala Yusoufzai, amewasili nchini
Uingereza kupata matibabu.
Malala
mwenye umri wa miaka 14 amewasili mjini Birmingham baada ya kufanyiwa
upasuaji nchini Pakistan kuondoa risasi mwilini mwake.
Madaktari wamesema itachukua muda mrefu kwa msichana huyo kuweza kupona majeraha ya kimwili na ya kisaikolojia.
Malala
alipata umaarufu baada ya makala aliyoandika kwa ajili ya shirika la
utangazaji la Uingereza, BBC, akielezea unyanyasaji unaofanywa na
wanamgambo wa Taliban.
Watu wasiojulikana walisimamisha basi aliyokuwa akisafiria kutoka shule na kumpiga risasi.