JE, WAJUA TAKRIBANI WANAUME 15000 DAR ES SALAAM HULALA NA MACHANGUDOA KILA SIKU.
Posted on
Oct 21, 2012
|
No Comments
Kwa mujibu wa utafiti wa Mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi nchini
–NACP, kwa kushirikiana na Wizara ya afya na ustawi wa jamii jumla ya
wanaume 15,000 wateja wa wanawake wanaojiuza (machangudoa) nchini.
Utafiti huo mpya uliofanyika kwenye wilaya tatu za Dar e Salaam,
Temeke, Ilala na Kinondoni umebaini kuwa wanawake wanaofanya biashara
ya ngono wanafikia 7,500 huku kila mmoja akiwa na wateja watatu kwa
siku.
Sababu ya kufanyika utafiti jijini Dar es Salaam ni kutokana na Idadi
kubwa ya watu na muingiliano wa tamaduni katika maeneo kadhaa zikiwemo
klabu za usiku, mahotelI na maeneo mengine yasiyo rasmi ambapo biashara
ya ngono hufanyika kwa kiasi kikubwa na kuashiria ongezeko maambukizi ya
ukimwi.
Pia matokeo ya ufuatiliaji wa wanawake wanaojiuza Dar es salaam pekee
umebaini kuwa kiwango cha maambukizi ni asilimia 31.4 ukilinganisaha na
asilimia 10.4 ya kiwango cha maambukizi kwa wanawake wote jijini Dar es
Salaam, lakini je hali hii ipoje kwa mikoa mingine?
