KAMISHNA WA UMOJA WA ULAYA AAMUA KUACHIA WADHFA WAKE BAADA YA KUKUMBWA NA KASHFA.
Posted on
Oct 17, 2012
|
No Comments

Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya Afya amejiuzulu kutokana na kashfa za rushwa.
Kamishna
huyo John Dalli kutoka Malta amechukua uamuzi wa kuachia madaraka hayo
baada ya kitengo cha Umoja wa Ulaya cha kupambana na ufisadi kugundua
kwamba mjasliamali kutoka Malta alitaka kutumia ushawishi alio nao kwa
kamishna huyo, kujipatia malipo kutoka kampuni ya sigara ya Sweden.
Mjasliamali huyo amedai kwamba angeweza kusimamisha sheria ya Umoja wa Ulaya inayohusu matumizi ya tumbaku.
Halmashauri
ya Ulaya ilisema haina ushahidi kwamba Dalli alihusika moja kwa moja
katika kashfa hiyo, lakini imesema inaamini kwamba alifahamu kilichokuwa
kikiendelea.-DW.