MISS EAST AFRICA 2012 TANZANIA YATANGAZA MREMBO WAKE.
Posted on
Oct 21, 2012
|
No Comments

Mrembo atakaewakilisha Tanzania katika mashindano ya mwaka huu ya Miss East Africa ni JOCELYNE DIANA MARO (22)
Mrembo
huyo alipatikana kufuatia mchakato ulioendeshwa na kamati maalum ya
kuratibu zoezi hilo kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita na kuwashinda
warembo wengine 148 waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss East Africa 2012
Jocelyne
amehitimu shahada ya Business Economics mwezi wa saba mwaka huu katika
chuo kikuu cha Keele University, Nchini Uingereza
Maandalizi
ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na yapo kwenye hatua za mwisho
ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zote za BASATA ili kufanikisha
mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi
wa Mlimani City Jijini Dar es salaam
Mashindano
ya Miss East Africa mwaka huu tayari yameanza kuvuta hisia za watu
wengi barani Africa kufuatia kiwango cha juu cha warembo wanaowania taji
hilo.
Nchi
zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja
na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja
na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano
ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni
wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi
wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.