TANZANIA YAIAMBIA MALAWI, FANYA UTAFITI WA MAFUTA LAKINI MARUFUKU UPANDE WA ZIWA WA TANZANIA
Posted on
Oct 21, 2012
|
No Comments
Tanzania
imesema Malawi inaweza kuendelea na utafiti wa mafuta katika kaskazini
magharibi ya Ziwa Nyasa, lakini marufuku kufanya utafiti huo nusu ya
upande wa kaskazini mashariki sababu huo ni eneo la Tanzania.
Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda aliiambia BBC, Alhamisi kwamba
kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Tanzania inamiliki nusu ya ziwa,
hivyo Malawi inaweza kuendelea kufanya utafiti al muradi utafiti huo
ufanyike upande wao na wasivuke mpaka, ambao ni katikati ya ziwa.
“Kama Malawi wanafanya utafiti, wafanye wakielewa kwamba kuna mpaka,
na hakutakua na tatizo. Lakini wanafikiria kupuuza mpaka, kauli yetu
kwao ni hapana, ziwa lote sio lenu” alisema PM Pinda.
Akijibu swali kwa nini askari wa Tanzania wanawasumbua wavuvi wa
Malawi ziwani, PM Pinda alisema kama wavuvi hao wa Malawi wamevuka mpaka
wa kimataifa, ambao ni katikati ya ziwa, askari wa Tanzania wana wajibu
wa kuwakamata na kuwahoji.
“Ni kweli tuliwahoji kwanini wameingia katika eneo la Tanzania, tukawaambia warudi katika upande wao wa ziwa” alisema.
Aliongeza kwamba Tanzania inataka kumaliza mgogoro wa mpaka kwa
amani. Na kwamba inataka amani ya muda mrefu kati ya nchi hizi mbili
iendelee.

