photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > WAKATI POLISI WAKITAWANYA WATU KWA MABOMU YA MACHOZI DARAJANI ZANZIBAR, DAR ES SALAAM HAMKANI SI SHWARI.

WAKATI POLISI WAKITAWANYA WATU KWA MABOMU YA MACHOZI DARAJANI ZANZIBAR, DAR ES SALAAM HAMKANI SI SHWARI.

Posted on Oct 19, 2012 | No Comments

Wakati Zanzibar Sakata la Waislamu kuendeleza kitimtim kufuatia kutoonekana kwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho Vurugu zimeendelea kutawala eneo la Darajani na kusababisha Polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu.
Jijini Dar es Salaam hali si tofauti na hiyo maeneo ya Kariakoo maduka kadhaa yamefungwa kufuatia vurugu kama hizo baada ya Swala ya Ijumaa kufuatia pia kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda yamekuwa ni matokeo ya vurugu watu kukimbizana huku Polisi wakidhibiti Usalama na Amani kuelekea harijojo.(Picha na Maktaba).
Maeneo ya Posta karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani Askari wameweka utepe wa kudhibiti watu kuingia katika maeneo hayo kitendo kilichosababisha shughuli nyingi kusimama.
Pichani ni Jeshi la Wananchi Tanzania likiwasilia maeneo ya Kariakoo kuongezea nguvu kwa ajili ya kutuliza ghasia. (Picha hii imepigwa na mdau Mpeli Jr Ngonywike kupitia mtandao wa facebook alipopiga picha hii kwa kujificha.
Pichani ni Vipeperushi  vilivyotolewa na Waumini wa Dini ya Kiislamu kabla ya maandamano leo.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru