>
SPORTS
>
YANGA YAITANDIKA RUVU SHOOTING MAGOLI 3-2 UWANJA WA TAIFA
YANGA YAITANDIKA RUVU SHOOTING MAGOLI 3-2 UWANJA WA TAIFA
Posted on
Oct 20, 2012
|
Mchezaji
wa timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam akimiliki mpira mbele ya beki
wa timu ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam,
mpira umekwisha timu ya Yanga imeifunga Ruvu Shooting magoli 3-2, Goli
la tatu la timu ya Yanga limepatikana katika kipindi cha pili cha
mchezo huo baada ya kutoka uwanjani kwa mapumziko zikitoshana nguvu kwa
kufungana magoli mawili kwa mawili katika kipindi cha kwanza
Mchezaji
wa Yanga Jerrison Tegete akishangilia mara baada ya kufunga goli la
pili katika mchezo huo na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika timu
zikitoshana nguvu kwa magoli, mpaka kipindi cha pili ambapo Yanga
iliongeza goli la tatu na kufanya matokeo hayo kuwa 3-2
Mashabiki
wa timu ya Yanga wakizikilizaia maumivu wakati timu yao ilipokuwa iko
nyuma kwa magoli 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya kukomboa magoli
hayo na kuongeza goli la tatu katika kipindi cha pili.