ASKARI POLISI, MAGEREZA HAWAJALIPWA MISHAHARA
Posted on
Nov 17, 2012
|
No Comments
Askari wa Jeshi la Polisi na
Magereza nchini hawajalipwa mishahara yao ya mwezi wa 10 mwaka huu hatua
inayowafanya wageuke kuwa ombaomba na wategemezi kwa ndugu na marafiki.
Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti jana, askari hao walisema kwa sasa wanaishi maisha ya shida kwa kuwa walizoea kupokea mishahara yao tarehe 25 ya kila mwezi, lakini mwezi uliopita haikuwa hivyo na mpaka jana baadhi yao walikuwa hawajlipwa.
“Ndugu yangu hatujalipwa mishahara ya mwezi uliopita na hatujui ni lini tutalipwa mishahara yetu. Tunaishi maisha ya shida ya kuombaomba kwa ndugu na washikaji zetu,” alisema mmoja wa maskari hao.
Askari hao walisema kuna wenzao waliopokea mishahara, lakini wengi wao hawajalipwa na kwamba, hawajui ni kwa nini walipwe kwa awamu wakati siku za nyuma walikuwa wanalipwa wote kwa wakati mmoja.
Akizungumzia madai ya askari hao, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga alithibitisha watumishi hao kutolipwa mishahara ya mwezi uliopita.
“Ni kweli baadhi ya askari wetu katika maeneo mbalimbali ya nchi mpaka leo hawajalipwa mishahara yao ya mwezi uliopota. Lakini hali hii imetokana na tatizo la kompyuta,” alisema Nantanga na kuongeza:
“Siku za nyuma mishahara ilikuwa inalipwa mkononi kwa baadhi ya askari, lakini hivi sasa mishahara yote inalipwa kupitia benki na utaratibu huu umekwamishwa na mtandao wa kompyuta.”
Alisema mishahara ya askari Magereza waliopo nje ya Dar es Salaam malipo yao yatafanyika katika ofisi ndogo za Hazina katika maeneo walipo na kwamba, mpaka sasa baadhi bado hawajalipwa.
Hata hivyo, alikanusha madai ya baadhi ya askari kwamba ucheleweshwaji huo wa msihahara umetokana na serikali kuishiwa fedha.
“Serikali haina tatizo la fedha. Ila tatizo hili limetokana na kuanzishwa utaratibu mpya wa kulipa mishahara kupitia benki. Na hili ndilo tatizo lililosababisha ucheleweshwaji huu na sio kitu kingine,” alisema Nantanga.
Alisema hana uhakika ni lini askari hao watalipwa mishahara yao na kuongeza kwamba, wizara yake inafanya kila jitihada ili kuhakikisha tatizo hilo linamalizika haraka na askari wote wanalipwa.