HIZI NI SENTENSI NNE ALIZOZISEMA ADEN RAGE KUHUSU KINAONDELEA SIMBA IKIWEMO ISHU YA JUMA KASEJA.
Posted on
Nov 18, 2012
|
No Comments
Wakati
kukiripotiwa kuwa na hali isiyo nzuri ndani ya makao makuu ya klabu ya Simba
kutokana na matokeo ya hivi karibuni kwenye ligi kuu Tanzania, mwenyekiti wa
klabu hiyo Aden Rage amekaa na kuzungumza na waandishi wa habari.
Alhaj Ismail Aden
Rage ambae ni mbunge wa Tabora mjini amesema anatambua kila kinachoendelea
ndani ya klabu kwa kusema kuwa wapo wanaosababisha hali hii itokee lakini yapo
mengi ambayo yamebadilika katika utawala wake.
Kwenye sentensi
ya pili amesema kwa niaba ya uongozi wa klabu ya Simba anapenda kuchukua fursa
hiyo kumuomba radhi nahodha na mlinda mlango wa klabu ya Simba Juma Kaseja
kwa yote yaliyomsibu baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo kwa sasa moja
kati ya mambo ambayo uongozi wake umepania kuyafanya ni kuitoa timu nje ya nchi
kwa matayarisho ya duru ya pili ya ligi kuu na mashindano ya kimataifa.
Rage pia
alizungumzia ishu ya kusimamishwa uanachama wanachama Ally Bane na Ustadh
Masoud kwa kile alichokiita kukiuka katiba ya klabu ya Simba kutokana na
walichofanya ikiwemo kuhamasisha wanachama wa Simba kutia saini ili kikao
cha dharura kifanyike kuokoa migogoro iliyopo kwenye klabu wakati huu.
Pia mwenyekiti huyo amevunja kamati ndogo zote alizoziteua kipindi kilichopita ambazo ni kamati ya mashindano inayoongozwa na Joseph Itang’are Kinesi, ya Ufundi iliyokuwa ikiongozwa na Ibrahim Masoud, kamati ya fedha iliyokuwa chini ya Geofrey Nyange Kaburu, kamati ya usajili iliyokuwa chini ya Zakaria Hanspope na kamati ya nidhamu.