KANISA LAVAMIWA; MAPADRE WAPIGWA RISASI IRINGA
Posted on
Nov 17, 2012
|
No Comments
Eofrey Nyang’oro, Iringa
MAPADRI wawili wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, Jimbo la Iringa, wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, kutokana na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuwajeruhi kwa silaha za jadi na bunduki, baada ya kuvamia nyumba wanazoishi.
Paroko wa Kanisa hilo Angelo Burgio kutoka Italia (60) na msaidizi wake Herman Myala walikumbwa na mkasa huo usiku wa kuamkia jana.
Padri Burgio alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mbili kifuani na kucharangwa mapanga, msaidizi wake Padri Myala alijeruhiwa kwa
mapanga na kuburutwa chini kwenye ardhi.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku moja tangu kuvamiwa kwa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa lililopo eneo la Kihesa mkoani humo, ambapo mlinzi wa kanisa hilo, Batholomea Nzigilwa (65) alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Nzigilwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, huku hali yake ikielezwa ikiwa ni mbaya.
Watangaza msamaha Jana gazeti hili lilishuhudia Padri Burgio akiwa amelazwa, huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji wakati akisubiri huduma ya upasuaji kwa ajili ya kutolewa risasi mwilini.
Akizungumza kwa tabu, padri huyo alisema majambazi hao walifika eneo la Kanisa la Kihesa saa tano usiku wakiwa na silaha mbalimbali
za jadi na bunduki.
Alisema baada ya kumshambulia msaidizi wake, walimfyatulia yeye risasi kifuani wakati alipofungua mlango na kutaka kukimbia.
“Mimi baada ya kuwasikia nilifungua mlango kwa lengo la kutaka kukimbia ili nijinusuru, lakini hamadi wakanifyatulia risasi kifuani. Nilianguka chini na walipoingia ndani walichukua fedha taslimu Sh3.5 milioni zilizokuwa chumbani kwangu na kisha kunikata na panga
kichwani, ” alisema Burgio.
Hata hivyo, padri huyo alisema, “Sisi tunawasamehe. Mimi na mwenzangu tumewasamehe tangu walipofanikiwa kutushambulia na kukimbia. Tunawaombea msamaha kwa Mungu kwani yeye ndiye anayejua,” alisema Padri Burgio.