TANESCO YAKATA RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA KUILIPA DOWANS.
Posted on
Nov 20, 2012
|
No Comments

Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) limekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa
Tanzania kuomba zuio la utekelezaji wa hukumu ya Mahakama Kuu,
inayolitaka kuilipa Shilingi bilioni 96 Kampuni ya kufua umeme wa
dharura ya Dowans.
Tanesco
wamekataka rufaa hiyo ili kusitisha utekelezaji wa hukumu ya Mahakama
ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), kama
ilivyoamuliwa na Mahakama Kuu, iliyolitaka shirika hilo liilipe Dowans
fedha hizo, ikiwa ni fidia ya kuvunja mkataba wa biashara kinyume cha
sheria.
Rufaa hiyo iliwasilishwa Septemba 19 na imepangwa kusikilizwa Desemba 5 mbele ya jopo la majaji watatu.
Katika rufaa hiyo, Tanesco inaomba kusitishwa kwa utekelezaji wa uamuzi huo hadi kesi ya msingi inayoendelea katika Mahakama ya Kimataifa Divisheni ya Biashara itakapokwisha.