Uganda inatarajia kupitisha sheria mpya dhidi ya ushoga kufikia mwishoni mwa mwaka huu, ikiwa kama zawadi ya ‘Christmas, kwa wahusika wa mahusiano ya jinsia moja.
Shirika la Habari la AP limemkariri Spika wa Bunge la nchi hiyo Rebecca Kadaga  (pichani) akisema wananchi wanahitaji sheria hiyo.
Vitendo vya kishoga ni marufuku na ni kinyume na sheria nchini Uganda na mswada wa suala hilo uliowasilishwa bungeni unapendekeza adhabu kali kwa watu watakaobainika.
Hata hivyo Wahisani wa nje wamekuwa wakitishia kusitisha misaada iwapo haki za mashoga nchini humo hazitatambuliwa.