VETTEL BINGWA WA DUNIA MARA 3 FORMULLA 1
Posted on
Nov 28, 2012
|
No Comments
Mjerumani Sebastian Vettel,
dereva wa timu ya magari ya Red Bull, aliibuka bingwa wa dunia,
alipoweza kuwazidi madereva wenzake kwa pointi tatu katika mashindano ya
Brazil ya langalanga siku ya Jumapili.

Dereva mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuwa bingwa wa dunia mara tatu mfululizo katika mashindano ya langalanga
Hii ni mara ya tatu mfululizo Vettel anaibuka bingwa wa dunia.
Katika
mashindano yaliyojaa matukio mbalimbali, ikiwa pia ni pamoja na mvua,
Vettel alipambana vikali kumaliza katika nafasi ya sita, kwani wakati
mmoja alipokuwa mwisho, baada ya ajali kufanyika katika mashindano hayo.
Mpinzani wake mkali zaidi msimu huu, Fernando
Alonso, wa timu ya Ferrari, alikamilisha mashindano akiwa katika nafasi
ya pili, na hayo yakimaanisha Vettel alihitaji kumaliza katika nafasi
sita za mwanzo ili kutangazwa bingwa.
Lakini mshindi wa mashindano hayo ya Formula 1 ya Brazil alikuwa ni Jenson Button, wa timu ya McLaren.
Button alimtangulia mwenzake wa timu ya Mclaren,
Lewis Hamilton, aambaye gari lake liligongwa na dereva wa Force India,
Nico Hulkenberg.
Mjerumani Hulkenberg alikuwa akijaribu kumpita
Hamilton ili aweze kutangulia, na zikiwa zimesalia raundi 27, lakini
hakuweza kulidhibiti gari lake vizuri, na liliteleza na kuligonga gari
la Hamilton.
Hulkenberg aliadhibiwa, na kumaliza katika
nafasi ya tano, nyuma ya mwenzake Alonso, Felipe Massa, aliyemaliza
katika nafasi ya tatu, na dereva wa Red Bull, Mark Webber, akiwa katika
nafasi ya nne.
Vettel, mwenye umri wa miaka 25, ndiye dereva
mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya mashindano hayo kuweza
kuandikisha ubingwa wa dunia mara tatu mfululizo.