XI ATHIBITISHA KIONGOZI MPYA WA UCHINA
Posted on
Nov 15, 2012
|
No Comments

Viongozi wapya wa Uchina
Xi Jinping amethibitishwa rasmi kuwa mtu ambaye ataiongoza Uchina katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Bwana Xi, aliongoza mkutano wa kamati kuu ya
chama cha Kikomunisti nchini Uchina maarufu kama Politburo uliofanyika
katika ukumbi wa baraja la mji mkuu wa nchi hiyo Beijing, hatua
inayoashiria kupandishwa kwake kuwa kiongozi wa chama hicho tawala.
Akiongea
wakati wa mkutano huo Bwana Xi alisema kuwa, chama hicho kinakabiliwa
na changamoto nyingi lakini atafanya kazi ili kuhakikisha kuwa ameafikia
matakwa na matarajio ya raia wa nchi hiyo.
Wengi wa viongozi wapya katika kamati hiyo
wanaonekana kuwa wanasiasa wahafidina na wale waliokisiwa huenda
wakaleta mabadiliko hawakupandishwa cheo.
Xi Jinping anachukua mahala pa Hu Jintao, ambaye chini ya utawala wake, uchumi wa Uchina umekuwa kwa kiasi kikubwa.
Hatua hiyo sasa imekalisha shughuli rasmi ya kukabithi madaraka ya nchi kwa kizazi kipya.
Baada ya mkutano huo kukamilika, Bwana Xi,
aliondoka kwenye ukumbi huo akifuatwa na Bwana Li Keqiang, ambaye
atamrithi Waziri mkuu wa nchi hiyo Wen Jiabao, na wanachama wengine
watano wenye ushawishi mkubwa katika kamati hiyo kuu ya chama, ambayo
awali ilikuwa na wanachama Tisa lakini imepunguzwa hadi wanachama Saba.
Watano hao ni pamoja na makama wa rais, Zhang
Dejiang, kiongozi wa chama hicho mjini Shangai, Yu Zhengsheng, afisa
mkuu anayehusika na masuala ya habari na propaganda Liu Yushan, Naibu
Waziri Mkuu
Wang Qishan na kiongozi wa chama cha Tianjin Zhang Gaoli.
Wang Qishan na kiongozi wa chama cha Tianjin Zhang Gaoli.
Viongozi hao wana majukumu makubwa na Bwana Xi,
amesema dhamira yao kuu ni kuunganisha na kuongoza chama hicho na
kuifanya taifa hilo kuwa thabiti na lenye ushawishi zaidi.