MESSI KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA KWA MARA YA 4??..
Posted on
Dec 3, 2012
|
No Comments

Christiano Ronaldo, Lionel Messi na Andres Iniesta wote wameorodheshwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka huu ya Ballon d’Or.
Messi
mshambuliaji wa Barcelona mwenye umri wa miaka 25, tayari ameshinda
mataji hayo mara tatu na bado anapigiwa debe kushinda tena tuzo hii
ambayo itatangazwa mjini Zurich mnamo Januari saba baada ya kura kupigwa
na waandishi habari, manahodha wa timu za taifa pamoja na makocha.
Kama
atashinda, anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kushinda taji hilo mara nne,
baada ya kujiunga na gwiji wa Ufaransa na rais wa sasa wa Shirikisho la
Soka Ulaya UEFA Michel Platini kama wachezaji pekee kushinda mara tatu
mfululizo. Nyota wa Uholanzi Johan Cruyff na Marco Van Basten pia
wamewahi kushinda matatu.
Mkufunzi
wa Uhispania Vicente del Bosque ambaye aliongoza timu yake kushinda
taji la UEFA EURO 2012 na kuwa wa kwanza kushinda vinyang’anyiro vitatu
mfululizo ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kutwaa tuzo ya kocha bora na
atapambana na Jose Mourinho wa Real Madrid na Pep Guardiola aliyekuwa
wa Barcelona.
Kwa
upande wa tuzo ya mchezaji bora kwa wanawake, bingwa mara tano wa
Brazil Marta atapambana na Wamarekani Aby Wambach na Alex Morgan.
