SHEREHE YA MIAKA 20 YA KLAB BILLICANAS NA 13 YA CLOUDS FM KWA PAMOJA
Posted on
Dec 3, 2012
|
No Comments

Sherehe hizo zilipambwa na shamrashamra za aina mbalimbali ikiwemo kukati keki pamoja na kufungua shampeni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group Dk. Lilian Mtei akizungumza katika hafla hiyo.

Mwakilishi wa Clouds FM, Wasiwasi Mwabulambo akizungumza katika hafla hiyo.

Dk. Lilian Mtei akikata keki.

Mmoja
kati ya wafanyakazi wa kwanza wakati Bilicanas Club inaanzishwa miaka
20 iliyopita, Monika Victor akimlisha keki, Dk. Lilian Mtei wakati wa
hafla ya kutimiza miaka 20 ya klabu hiyo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.

Monica Victor akigawa keki kwa wadau waliofika katika sherehe hizo.

Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa na mmiliki wa blog ya Bongoweekend, Khadija Kalili pamoja na wadau wengine.

Bendi
ya muziki ya dansi ya Sky Light ikitumbuiza katika sherehe za kutimiza
miaka 20 ya Club Bilicanas na miaka 13 ya Clouds FM.

Watu wa mataifa mbalimbali wakicheza muziki katika ukumbi wa Bilicanas.
Wadau
mbalimbali wa burudani wamefurahia kwa pamoja na kula keki ya miaka
20 ya klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka 13 ya Clouds Fm,
iliyoambatana na shamrashamra mbalimbali ndani na nje ya ukumbi huo.
Sherehe
hizo ziliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group Dkt. Lilian
Mtei ambapo amewashukuru wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu
hiyo, tangu 1992.
Amesema “Tunawashukuru sana kwa kuwa nanyi mara zote inatia faraja kwetu na tutaendelea kutoa huduma bora siku zote”.
Dkt.
Mtei pia amewashukuru wafanyakazi mbalimbali waliofanikisha ukumbi huo
kufikia hapo na kutoa heshima ya kipekee kwa wafanyakazi waliokuwapo
tokea inaanza hadi ilipofikia miaka 20 na hatimaye kukata keki hiyo.
“Uwepo
wa miaka 20, tuna kila sababu ya kuwapongeza wafanyakazi tuliokuwa nao
toka mwanzo hadi sasa, na kwa heshima ya pekee Mama Victor na Mrs.
Mitemo ndiyo watakao kata keki hii” alisema. Mtei.
Keki
hiyo ilikatwa na wafanyakazi hao Monica Victor na Pili Mitemo
ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo,
ambaye kwa sasa ni marehemu.
Aidha,
kwa upande wa Clouds FM, iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye
alipongeza klabu Bilicanas kwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua sanaa
nchini hasa kwa kuwasaidia wasanii kufikia malengo yao.
Kwa
upande wake Ibrahim Tuwa ‘Dj Ibra’ aliyekuwa akisherehesha shughuli
hiyo, aliwaomba wadau kuendelea kuwaunga mkono na kuwa wataendelea na
huduma bora zaidi ya hapo.
Dj
Ibra alijiunga na Bilicanas tokea 2002, ambapo mpaka sasa ana miaka 10
kwenye klabu hiyo iliyowahi kuwa na madj maarufu waliopita hapo ambao
wengi wao wapo kwenye vituo vya televisheni na redio.
