HUYU NDIYO MBUNGE WA CHADEMA ANAYESAKWA NA POLISI
Posted on
Mar 8, 2013
|
1 Comment
Arusha.Polisi Mkoa wa Manyara inamsaka Mbunge wa Viti wa Mkoa wa Manyara(Chadema ),Rose Kamili pamoja na watu wengine wanne kwa tuhuma za kufunga ofisi ya kijiji cha Basotu kwa zaidi ya wiki moja sasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa wanamsaka mbunge huyo,pamoja na wenzake ili watowe maelezo kuhusiana na tukio hilo kabla ya kufikishwa mahakamana.
Mbunge Kamili alipoulizwa jana kuhusiana na kusakwa huko, alikiri kupata taarifa lakini akasema,kama polisi wanamuhitaji wamfuate nyumbani kwani wanapajua.
Hata hivyo, alisema uamuzi wa kufungwa ofisi hiyo, yalitolewa kwenye mkutano wa mkuu wa kijiji,kutokana na kupinga unyanyasaji wa viongozi wa kijiji, kutosoma mapato na matumizi tangu mwaka 2007 na pia kuwataka wafike Basotu viongozi wa wilaya.
Wananchi 365 walioshiriki mkutano mkuu huo wa kijiji, licha ya kufunga ofisi hiyo pia walichagua vijana waliopitia mafunzo ya mgambo kulinda ofisi hizo hadi muafaka utakapopatikana.

Hi there just wanted to give you a quick heads up. The words in your post
ReplyDeleteseem to be running off the screen in Opera. I'm not sure if this is a format issue or something to do with browser compatibility but I figured I'd post to let you know.
The style and design look great though! Hope you get the
issue resolved soon. Thanks
Here is my blog :: Spotduck.com