INDIA YASIMAMA KIDETE YAMZUIA BALOZI WA ITALIA ASIONDOKE NCHINI HUMO MPAKA KIELEWEKE
Posted on
Mar 14, 2013
|
No Comments

Mahakama Kuu nchini India imeamuru balozi wa Italia nchini humo asiondoke, kufuatia Rome kukataa kuwarejesha India askari wake wawili wa majini wanaokabiliwa na tuhuma za mauaji ya wavuvi huko Kerala mwaka jana.
Mahakama hiyo ilikuwa imewaruhusu askari hao wa majini kujea kwao kupiga kura katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Balozi huyo Daniele Mancini yeye mwenyewe alikuwa ameihakikishia mahakama hiyo kuwa askari hao watarejeshwa India Machi 22 mwaka huu.
Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh ametahadharisha kuwa kutakuwa na matatizo vinginevyo Italia iwarejeshe askari hao.
Akitumia lugha kali, Waziri Mkuu huyo amesema kitendo cha kukataa kwa Italia kuwarejesha askari hao hakikubaliki.