MWANAFUNZI UDSM AJINYONGA HADI KUFA.
Posted on
Mar 26, 2013
|
2
Comments
Mwanafunzi wa kiume wa mwaka wa pili sheria mwenye umri kati ya 22 mpaka
25 amejinyonga.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa pili Kitivo
cha Sheria, Joseph Bernadina (25), amejinyonga kwa kutumia kamba na
kukutwa ameifunga juu ya mti, katika eneo la Yombo chuoni hapo.
Makamu
Mkuu wa Chuo hicho, Utawala, Profesa Yunus Mgaya, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba alipata taarifa hizo jana asubuhi.
Aliongeza
kuwa Jumamosi iliyopita alipokea simu kutoka kituo cha polisi cha chuo
hicho akielezwa kuwa kuna mwanafunzi alitishia kujiua, lakini
aliwahishwa hospitali na kupatiwa ushauri kutoka kitengo maalum cha
washauri wa chuoni hapo na kuruhusiwa Jumapili.
“Nilikuja tena
kushituka leo asubuhi napokea simu kutoka kwa mshauri wa wanafunzi kuwa
kuna wanausalama wamemkuta mwanafunzi akiwa amejinyonga juu ya mti huku
akiwa na karatasi kwenye mfuko wa sharti ikimtambulisha pamoja na ujumbe
uliosema, kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote kwani amejiua kwa
ridhaa yake --asisumbuliwe mtu yeyote kwani nimefanya hivi kwa maamuzi
yangu mwenyewe pia nizikwe kwetu--” alisema.
Profesa Mgaya
alisema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na Uongozi wa chuo kwa
kushirikiana na ndugu wa marehemu na kwamba Chuo kitagharamia
kuusafirisha mwili kama alivyoomba katika ujumbe aliouacha wa kupelekwa
wilayani Ludewa Mkoa wa Iringa.
Naye rafiki wa marehemu, Daniel
Mwamlima, alisema marehemu hakuwahi kuzungumza chochote kilichoashiria
kuwa ana matatizo wala mgogoro na mtu yeyote. Alisema walimuacha
hospitalini Jumamosi na kesho yake kumchukua, lakini baadaye
aliwatoroka.
“Sasa leo (jana) asubuhi tulipata taarifa za mwanafunzi kujinyonga mbaya zaidi tukakuta ni yeye,” alisema Mwamlima.
Waziri
Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO), Yasini Athumani,
alisema wamezipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa
tukio na alisema uchunguzi wa awali umebaini kwamba marehemu aliwahi
kuwa na historia ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya
kupata matibabu ya ugonjwa wa msongo wa mawazo.



Heya i'm for the first time here. I found this board and I in finding It truly helpful & it helped me out much. I hope to present something again and aid others such as you aided me.
ReplyDeleteAlso visit my blog post ... Nathen Jahiem
Please let me know if you're looking for a article author for your blog. You have some really good posts and I think I would be a good asset. If you ever want to take some of the load off, I'd absolutely
ReplyDeletelove to write some material for your blog in exchange for a link back to mine.
Please shoot me an e-mail if interested. Thanks!
Feel free to visit my website: Trever Jaime