UCHAGUZI KENYA; UHURU KENYATTA NA RAILA ODINGA BADO MISHE MISHE.
Posted on
Mar 5, 2013
|
No Comments
Kura zikihesabiwa kwenye kituo kilichopo Viwanja vya Kibera Social,
jijini Nairobi baada ya wananchi wa Kenya kupiga kura katika uchaguzi
mkuu wa nchi hiyo jana.

Raila Odinga wa chama cha ODM amepata kura 1,393,000 ni 41.00% ya kura zote zilizohesabiwa,
Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha kuwa Uhuru Kenyatta, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta anaongoza, huku akifuatiwa kwa karibu na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Raila Odinga.
Kama alivyo Uhuru, Raila pia ni mtoto wa mmoja wa
waasisi wa taifa la Kenya, ambaye alikuwa Makamu wa Mzee Kenyatta,
Jaramong Oginga Odinga.