photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > KITAMBULISHO CHA URAIA CHA KUVUKIA MIPAKA

KITAMBULISHO CHA URAIA CHA KUVUKIA MIPAKA

Posted on Jan 3, 2014 | No Comments



Wananchi wa mataifa ya Rwanda, Uganda na Kenya wamepokea kwa shangwe kuanza kwa mpango wa kutumiwa kwa vitambulisho vya uraia kama cheti cha kuwaruhusu kuvuka mpaka na kuingia moja wapo wa nchi hizo.


Mpango huu wa kutumia vitambulisho vya uraia kama pasi katika nchi hizo tatu umeanza kutumiwa rasmi tarahe Mmoja Januari kufuatia makubaliano kati ya viongozi wa mataifa hayo.

Taarifa zinazohusiana

Kenya
Rwanda

Mpango wenyewe unatokana na makubaliano kati ya viongozi wa nchi tatu waliouafikia wakati wa mkutano uliofanyika nchini Uganda mwezi Juni mwaka jana.

Kadhalika mpango huu unanuiwa kurahisisha usafiri wa watu wa jumuiya katika mataifa wanachama kama awamu ya pili ya ushirikiano kati ya mataifa wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo siku moja tu baada ya kuanzishwa kwa mpango wa kutumiwa kwa vitambulisho vya uraia kama cheti cha kuwaruhusu raia wa nchini tatu, Uganda, Kenya na Rwanda kuvuka mpaka na kuingia mojawapo wa nchi hizo sasa inaonekana mpango huo huenda ukawanufaisha watu wachache peke yake.

Sio raia wote wa Uganda , Kenya au Rwanda wanafahamu hayo . Wengi nchini Rwanda bado waliwasili katika mipaka ya nchi hiyo wakiwa wamejihami kwa Passpoti zao ili waweze kuruhusiwa kuvuka na kuingia katika nchi jirani. Hali ni hiyo hiyo nchini Uganda.

Baadhi hata hivyo wanahisi ingekuwa vyema kama mpango huu pia ungewafaidi watu wa Burundi, na Tanzania.

Kwa sasa ni raia wa Rwnada na Tanzania peke yao ambao wana vitambulisho vya kitaifa ikimaanisha kuwa raia wa Uganda watalazimika kutumia kadi zao za kupigia kura hadi taifa hilo litakapoanza kutoa vitambulisho.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru