Hii ni true story ambayo ilimtokea dada mmoja huku mkoani mbeya...
Alikuwa ni msichana ambaye kimwonekano alikuwa akionekana ni mrembo sana, japo sio ule urembo ambao uliwafanya vijana wengi wa mtaa aliokuwa akiishi kumsumbua. Zena ndilo jina lililokuwa likifahamika sana na baadhi ya watoto katika mtaa wa isanga ambako ndiko alikokuwa akiishi pamoja na wazazi wote wawili. Baba yake ambaye alikuwa ni mwenyeji wa kyela, huku kabila lake likiwa ni mnyakyusa. Mzee mwakitalima ndilo jina lililokuwa likifahamika sana na baadhi ya watu katika mtaa huo. Mzee huyo licha ya kufahamika pia alikuwa akisifika kwa ukali aliokuwa nao kiasi kilichofanya pia vijana wengi kumuogopa. Mara nyingi ilikuwa ni kawaida kusikia sauti ya kilio ikitoka katika nyumba hiyo ambayo iliashiria kuwa alikuwa akipigwa. Zena siku zote alikuwa akimuogopa baba yake huyo ambaye alionekana kama ni nyoka kwake. Siku zote alikuwa akimpenda mama yake ambaye hakuwahi hata siku moja kumpiga kwa fimbo. Siku zote alikuwa akifurahi ni kipindi ambacho baba yake alikuwa akisafiri na kubaki na mama yake ambapo nae alikuwa akiona ndo muda wa kutesa. Alikuwa akienda kucheza na wenzake nje ambapo kila mmoja alivyokuwa akimwona nje alikuwa akijua tu kuwa baba yake hayupo,kwani mara baba yake arudi alikuwa akishinda ndani huku akisoma kwani mzee mwakitalima alikuwa hana mchezo kwenye elimu.
* * * *
Zena alianza darasa la kwanza katika shule ya msingi mapinduzi iliyokuwa ikipatikana mita chache kutoka eneo alilokuwa akitoka. Alianza kusoma huku akiwa na maendeleo mazuri kitaaluma japo hakuwahi kushika nafasi ya kwanza ila siku zote alikuwa akikamata nafasi kumi za juu.
* * *
Miaka ilizidi kwenda na ndipo zena akafika darasa la tano katika shule hiyo ya mapinduzi. Katika miaka yote aliyosoma hapo shuleni wanafunzi wengi walikuwa wakishangaa ni kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo na kijana mmoja ambaye...
Itaendelea...
je ni kijana gan huyo? Itaendelea week ijayo..
Na Frank Philimon Ngobile