MATUKIO MBALIMBALI YA AJALI YA MV SKAGIT KATIKA BANDARI YA MALINDI ZANZIBAR LEO
Posted on
Jul 18, 2012
|
No Comments
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiwa na Viongozi Wakuu wa Serikali alipofika katika Ofisi za Shirika la Bandari, Malindi Unguja kupata taarifa sahihi ya ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Sky Get ikitokea Dar es Salaam kuelekea Unguja.
Wakazi wa Zanzibar wakiwa wamekusanyika katika Bandari ya Malindi mjini Unguja Zanzibar jioni ya leo wakati miili ya baadhi ya abiria wa Boti ya Kampuni ya Seagull "MV Skagit" wakitolewa baada ya boti hiyo kuzama na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200 hii leo ikitokea jijini Dar es Salaam.
Moja ya maiti ikiwa imebebwa na askari
Ni hali ya huzini Visiwani humo na jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla. Ajali hii imetokea ikiwa imepita miezi kadhaa baada ya meli nyingine ya Abiria kupoteza uhai wa watu visiwani humo.
Meli ya Mv Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar imezama majira ya saa nane mchana hii leo katika maeneo Pungume na Chumbe baada ya kukumbwa na upepo mkali.
Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia upande mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na jitihada mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya Bandari na vyombo vyengine.
Mpaka tunandika taarifa hizi ni maiti tatu zilikwishapatikana na kiasi cha abiria 150 wameokolewa na waliojeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya Mnazimmoja.
Taarifa zinaeleza kwamba kulikuwa na watoto takriban 30 na Watalii kutoka nchi mbali mbali wafikao kumi.
Wazamiaji kutoka Kikosi cha KMKM pamoja na Jeshi tayari wapo eneo la ajali kusaidia kuokoa maisha ya wananchi waliokumbwa na maafa haya.