KANISA LA POLISI LASHAMBULIWA GARISSA
Posted on
Nov 4, 2012
|
No Comments
Polisi nchini Kenya wanasema watu kama 7 wamejeruhiwa kwenye shambulio la guruneti dhidi ya kanisa katika mji wa Garissa.
Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya
na televisheni ya Kenya, KTN, wanasema idadi ya watu waliojeruhiwa
inaweza kuwa kubwa zaidi na baadhi ya majeruhi ni mahatuti.
Afisa mmoja amesema kanisa hilo lilikuwa ndani ya kambi ya polisi na guruneti liling'oa paa wakati wa ibada.
Wengi waliojeruhiwa ni askari polisi.
Mji wa Garissa uko karibu na mpaka wa Somalia.
Mwezi wa Julai watu 15 walikufa katika mashambulio kama hayo dhidi ya makanisa mjini Garissa.