photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > Joseph Mbowe wa NECTA asimamishwa kazi; Waisalam waandamana Dar es Salaam

Joseph Mbowe wa NECTA asimamishwa kazi; Waisalam waandamana Dar es Salaam

Posted on Jun 8, 2012 | No Comments



Afisa Uhusiano wa Baraza la Mitihani la Tanzania, John Nchimbi, akizungumza katika kipindi cha Jahazi cha redio CloudsFM amethibitisha ukweli wa taarifa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Dkt. Joyce Ndalichako ametoa barua aliyoitia saini ambayo inapaswa kusambazwa kwa vyombo vyote vya habari inayotaarifu kusimamishwa Kazi kwa Mkuu wa Tathmini na Kitengo cha Computer, ndugu Joseph Elias Mbowe.
Wakati huo huo, licha ya Serikali kuzuia kufanyika kwa maandamano ya Waislam kufuatia malalamiko yao dhidi ya NECTA kuhusu matokeo ya somo la Islamic Knowledge kukosewa kwenye matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita, leo hii Waislam kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wameandamana kuishinikiza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa ajiuzulu na kuitaka Serikali ivunje Baraza la mitihani.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru