Naibu Waziri, Nyalandu afungua maonyesho ya KARIBU FAIR 2012 leo..
Posted on
Jun 8, 2012
|
No Comments
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu leo mchana amezindua rasmi maonesho makubwa ya sekta ya Utalii ya Karibu mjini Arusha. Baada ya kuwasili katika viwanja vya Maonesho, Nyalandu alipata wasaha wa kuzungumza na viongozi wa TTB, TATO pamoja na waandaji wa Karibu Fair 2012.
Nyalandu akipata maelezo ya kampuni inayotoa huduma za helikopta hapa Tanzania ya Whirlwind. Anayempa Maelezo ni Capt. Neels ambaye alisema kampuni yake ipo mbioni kuleta helikopta 5 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Madhumuni ya mpango huo ni kuzitawanya katika maeneo mbalimbali ya nchi hii ili ziweze kutumika kwenye huduma za dharura haraka pale zinapohitajika. Sasa hivi wana helikopta moja nchini.
Mojawapo ya sababu ya ziada ya kuzuru maonesho ya Karibu Fair 2012 mkoani Arusha katika Viwanja vya Magereza (karibu na Arusha Airport) ni kujionea hema la orofa. Hema hili hutumika kwa malazi ya wageni wanapokuwa porini, hususan kwa wanaopenda kuweka kambi na kuacha kulala kwenye mahoteli. Moja ya makampuni yanayoshiriki Karibu Fair 2012 imeamua kuwaonyesha wageni na wadau bidhaa hii. Hema hili linahamishika.
