KELVIN YONDANI AKATA MZIZI WA FITINA
Posted on
Jun 22, 2012
|
No Comments
Kevin Yondan "Vidic".
Hatimaye aliyekuwa beki wa kutumainiwa wa klabu ya Simba katika msimu uliopita Kevin Yondan "Vidic" leo amekata mzizi wa fitina baada ya kuanza rasmi mazoezi katika uwanja wa Kaunda uliopo Makao Makuu ya klabu ya Yanga na kuwa kivutio katika mazoezi hayo.
Kipenzi hicho cha Yanga kiliwasili majira ya saa tatu kasoro dakika kumi asubuhi, ambapo mara baada ya kushuka katika gari mashabiki waliofurika katika mazoezi hayo walipomuona ghafla walimshangilia kwa vifijo na nderemo huku akielekea uwanjani…

