MTALII AWAWA NA MAJAMBAZI SERENGETI
Posted on
Jun 22, 2012
|
No Comments
Inasikitisha sana kusikia kwamba mtalii aliyekuja kupumzika Tanzania na kufurahia vivutio vya maliasili amekatishwa maisha yake hapa Tanzania, haitasahaulika milele kwa wanafamilia na nchi atokako. Majambazi waliovamia kambi/camp huko Serengeti na kupora familia 17 wamemuua mtalii mmoja toka Netherlands. Ni wakati muafaka kuimarisha huduma katika mbuga zetu za wanyama, kwani huingizia serikali mapato makubwa. Kwa tukio hili naamini kabisa ni headline kwenye nchi za Ulaya, na hii inaweza ikapunguza kabisa mapato yanayotokana na utalii. Serikali ifanye juu chini kuwapata wahalifu hawa, hata kama wanatoka nchi jirani. Pia nashauri serikali/hifadhi iwajibike kwa makosa haya ya kushindwa kutoa hifadhi iliyopaswa. Igharamie na kurudisha fedha ambazo wameporwa. Hili na liwe fundisho katika industry hii ya utalii.
