photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> KUTOKA BUNGENI: WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AMETANGAZA KUSITISHA KUTOA TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI NCHINI.

KUTOKA BUNGENI: WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AMETANGAZA KUSITISHA KUTOA TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI NCHINI.

Posted on Jun 28, 2012 | 1 Comment

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kusitisha Serikali kutoa tamko lake  kuhusu mgomo wa madaktari, ambao ulitakiwa kutolewa leo kama alivyoahidi jana Bungeni. Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu, Pinda, alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua Serikali ina mipango gani ya dharula ya kuumaliza mgomo huo. Alisema kwa hivi sasa, Serikali imechukua dharula, kwa kuwaita madaktari wasitaafu kwenda kwenye baadhi ya Hospitali za Serikali, kushika nafasi maeneo ambayo madaktari waliogoma. Vilevile Serikali imewataka wananchi waende kuhudumiwa kwenye hospitali za Jeshi, ikiwemo Lugalo. Pinda ameseama kuwa hata yeye alipopokea taarifa kuwa Dk. Ulimboka ametekwa na kupigwa alisikitika sana, na anamuombea apone haraka ili waendelee na suluhisho la mgomo huo wa madakatari. Alisema kuwa amemuagiza, Waziri wa Mambo ya ndani kuunda jopo la wataalamu kuchunguza kwa haraka kuhusu tukio hilo.

Comments:1

  1. HAPA HATUNA WAZIRI MKUU, HUYU JAMAA NI HOPELESS KABISA HUWAGA ANAONGEAGA PUMBA TU. MATAMKO YAKE MENGI UWA ANANYAMAZISHWA NA BOSI WAKE KWA VILE ANAKURUPUKA KUYATOA BILA KUFUATA TARATIBU. ALISHAWAHI KUROPOKA KUHUSU JAIRO, NA JANA KAROPOKA KUHUSU MADAKTARI YOTE HAYO ANAZIMWA. JIPANGE BABA MAANA UMEFELI KABISA HICHO KITI CHA PM.

    ReplyDelete