photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> TUCTA YAITAKA SERIKALI KUTOA TAMKO KUHUSU KIMA HALISI CHA MSHAHARA KWA SEKTA BINAFSI.

TUCTA YAITAKA SERIKALI KUTOA TAMKO KUHUSU KIMA HALISI CHA MSHAHARA KWA SEKTA BINAFSI.

Posted on Jun 28, 2012 | No Comments


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Nicholas Mgaya akizungumzana waandishi wa habari ambapo amesema kwa mujibu wa majadiliano ya Serikali walikubaliana kiundwe chombo cha pamoja kitakachoendesha utafiti kubaini kima halisi cha mishahara kwa sasa na uwezo wa Serikali kulipa.
Aidha Majadiliano hayo yaliwafikisha mahali ambapo vyama vya Wafanyakazi vilikubaliana kuwa kwa sasa wakati utafiti huo ukiendelea, kima cha chini cha mishahara kwa Watumishi wa Umma kisipungue Shilingi 200,000 kwa mwezi.
TUCTA inatarajia Bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma itakyosomwa Bungeni itatangaza kima cha chini cha Mshahara kisichopungua shilingi 200, 000 kwa mwezi.
Aidha Wameitaka Serikali itoe tamko kuhusu kima halisi cha mshahara kwa sekta binafsi

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru