Made in Africa; Zambibikes
Posted on
Jun 4, 2012
|
1 Comment
Imezoeleka kuona bidhaa nyingi za kutoka nje ya nchi zikiandikwa made in China au made in NY n.k. Nchini Zambia, wazambia wawili na wenzao wamarekani wawili, wameanzisha kiwanda kinachotengeneza baiskeli zinazoitwa "Zambibikes" zitokanazo na miti ya mianzi ( Bamboo) ambazo wanazisambaza duniani kote. Wenyewe wanasema"It's a plus to have a product that is grown in Africa, made in Africa and exported to everywhere else in the world,"
Spethmann, McBride, Chikamba, na Gershom Sikaala ambao ni waanzilishi wa kiwanda cha kutengeneza baiskeli, kwa kiasi chake wameweza kupunguza wimbi la vijana ambao hawana ajira Zambia kwa kuwaajiri kwenye kiwanda chao ambapo bidhaa zao husambazwa Japan, Singapore, Germany, Brazil, Finland na Marekani.


Hongera sana Zambia, u r leading the way to an independent state..
ReplyDelete