Msafara wa balozi wa uingereza nchini Libya washambuliwa..
Posted on
Jun 12, 2012
|
No Comments
Msafara wa balozi wa Uingereza nchini Libya umeshambuliwa kwa guruneti katika mji wa Benghazi uliopo Mashariki wa nchi hiyo.
Katika shambulio hilo walinzi wawili wa balozi huyo wamejeruhiwa.
Washambuliaji waliushambulia msafara huo mita kadhaa mbele ya ubalozi huo mjini Benghazi na kuvurumisha kifaa cha kulipuka kulilenga gari moja lililokuwa katika msafari huo.
Shambulio hilo lilikuwa la nne katika kipindi cha miezi mitatu dhidi ya ubalozi wa kigeni mjini humo.

