photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> NCCR-MAGEUZI acheni kupiga mayowe,acheni umma uone wenyewe.. !

NCCR-MAGEUZI acheni kupiga mayowe,acheni umma uone wenyewe.. !

Posted on Jun 4, 2012 | No Comments

Ndugu zangu,
NCCR- Mageuzi wamewajia juu wapinzani wenzao, Chadema. Wanawashutumu Chadema kwa kuwaita NCCR- Mageuzi ' CCM 'B'!
Tumemsikia Mbunge Machali akionyesha machachali yake ya kisiasa. Naye amewaita Chadema ' mahayawani' Neno ' hayawani' lina maana ya ' mnyama'- mtu kuitwa hayawani ina maana ya mtu ' mshenzi'- usiyestaaribika kama alivyo mnyama. Nalo ni tusi, si ajabu nao Chadema wakaja na kauli ya kuwataka NCCR- Mageuzi wawaombe radhi kwa kuwatukana hadharani!
Lakini tuanze na aliyeanza; Machali wa NCCR- Mageuzi anasema; Chadema, ama wawaombe radhi hadharani vinginevyo NCCR - Mageuzi inaweza kuwapeleka mahakamani. Ndio, kiduku cha kisiasa kimechanganya . Naam, siasa ni burudani pia.
Nionavyo, NCCR- Mageuzi hawana sababu ya kutoka na kupiga mayowe hadharani. Walichopaswa ni kufanya kinyume chake, kuwaimbia…

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru