Mkutano wa Maspecialist MNH, MUHAS NA ORCI ndo umekwisha na wameamua kuungana rasmi na madaktari wote nchini katika mgomo na kusitisha utoaji wa huduma zote zikiwemo za dharura Pia wanatoa wito kwa maspecialist wengine kote nchini kuungana katika mgomo huu. Pia wanalaani vikali vitisho na manyanyaso yanayofanywa na vyombo vya dola (serikali) dhidi ya madaktari na wameitaka serikali kutoa tamko la kuwahakikishia usalama madaktari kote nchini. Pia kuna haja ya kuweka modality ya kumsafirisha Dr. Ulimboka kwenda nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu zaidi zinahitajika $40,000( sawa na takribani tsh milioni sitini na nane 68000000). Na njia nyingine zote za uchangiaji pesa zimesitishwa na kupendekeza zitumike namba za mawakala zifuatazo Voda 31915 na Tigo 05416. (Chanzo kamati kuu ya jumuiya ya madaktari Tanzania).