Uongozi wa kampuni ya Vodacom Tanzania wakutana na spika wa bunge Anne makinda na kamati ya Miundombinu mjini Dodoma..
Posted on
Jun 12, 2012
|
No Comments
Spika wa Bunge Bi. Anna Makinda kulia akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza na Ofisa mahusiano Mkuu wa Vodacom Mwamvita Makamba. Viongozi wa Vodacom walipomtembelea Spika ofisini kwakwe mjini Dodoma leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Ofisa Mkuu wa Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba wakiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya Bunge ya miundombinu. Vodacom ilikutana na kamati hiyo leo mjini Dodoma kujitambulisha na kuzungumzia uwekezaji wa Vodacom nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Peter Serukamaba akiongoza kikao cha pamoja kati ya kamati yake na uongozi wa kampuni ya Vodacom Tanzania iliyotembelea kamati hiyo leo mjijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumzia uwekezaji wa Vodacom nchini. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza akifuatiwa na Ofisa Mkuu Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba

