photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> WALIMU WOTE KUANZA MGOMO JUMATATU TAREHE 01/07/2012.

WALIMU WOTE KUANZA MGOMO JUMATATU TAREHE 01/07/2012.

Posted on Jun 27, 2012 | No Comments

Uongozi wa kamati maalum ya kudai haki na maslahi ya walimu kupitia CWT- Chipolopolo; kwa huzuni kabisa tunapenda kuutanfazia Umma kuwa tarehe 01/07/2012 siku ya Jumatatu Walimu wote wa shule za sekondari na shule za Msingi wanakwenda kuanza mgomo wa siku tano kuishinikiza Serikali kuongeza mishahara ya Walimu kuendena na gharama za maisha na inflation. ( Katika mgomo huu walimu wote mnapaswa kushiriki pasipo uoga wowote kwani kwa pamoja tunaweza)

Maombi maalum

1. Tunawaomba wanafunzi wote wa sekondari na msingi wa tuunge mkono kwa siku tano hizo
2. Wazazi wote na wadau wa elimu tunaomba mtuunge mkono katika mgomo wetu ili kuboresha elimu ya watoto wetu
3. Likizo za wanafunzi zitanza kati ya tarehe 7 au 9 Julai hivyo huataathiri mgomo huu
4. Mgomo usio na kikomo kama serikali dhaifu itaendelea kuwa jeuri utafanyika tarehe 16/08/2012 kama ulivyopangwa lakini huu wa tarehe 1/7/2012 ni Pre mgomo kabla shule hazijafungwa na wanafunzi hawajamaliza mitihani na kupata matokeo yao


Walimu tunawajibu wakuitoa ujinga serikali kwa kushiriki mgomo huu pamoja twaweza


Upadate

1.kama Mgomo hautafanikiwa Walimu wote hawatashiriki kutoa na kusahisha mitihani ya nusu muhula ya kwanza
2.Walimu wote kutoshiriki zoezi la sensa ya Watu na Makazi kama wakusanya takwimu

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru