photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > WAZIRI SIMBA; AZINDUA BODI YA TAIFA YA URATIBU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YA AWAMU YA TATU

WAZIRI SIMBA; AZINDUA BODI YA TAIFA YA URATIBU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YA AWAMU YA TATU

Posted on Jun 28, 2012 | No Comments

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Sofia M. Simba amezindua Bodi ya Taifa ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya kipindi cha awamu ya tatu kwenye Mkutano wa uliofanyika Hoteli ya Dodoma, Mkoani Dodoma tarehe 28 Juni, 2012. Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Waziri Sofia Simba alimshukuru Mwenyekiti wa Bodi aliyemaliza muda wake, Dkt. Natu E. Mwamba kwa uongozi mzuri, na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza nchini kushika nafasi ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania wakati akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya NGOs.
Waziri Simba alieleza kuwa, Bodi iliyotangulia imeweza kufanya majukumu makubwa katika kipindi cha awamu ya pili kwa kuweza kusimamia kikamilifu uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kutoa mchango mkubwa katika utetezi wa makundi maalum, kutoa ushawishi wa kisera na  kutoa huduma za kijamii kama vile elimu, afya, chakula na malazi. Mchango wa NGOs hapa nchini umehamasisha Watanzania kushiriki kuchangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Bodi ya Taifa ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni chombo kilichoanzishwa chini ya Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005. Majukumu ya Bodi yameainishwa katika fungu la 7 la Sheria hiyo.  Baadhi ya majukumu haya yametekelezwa kwa kiwango kikubwa katika awamu mbili za Bodi zilizotangulia. Na inatarajiwa kuwa Bodi hii ya sasa itabiliana na changamato zilizopo ili kuendeleza Sekta ya NGOs kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii ya kitanzania. Waziri amesisitiza kuwa tayari kuhakikisha kuwa sekta hii ya NGOs nchini inakuwa na taaswira nzuri katika kuleta ari ya kuwajibika na kujituma kwa makundi yote kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru