FIGO ZA DKT. ULIMBOKA ZAANZA KUFANYA KAZI.
Posted on
Jul 3, 2012
|
No Comments
![]() |
| Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka. |
| AFYA ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imeendelea kuimarika baada ya kupata matibabu nchini Afrika Kusini na sasa figo zake zimeanza kufanya kazi.Dk Ulimboka alipelekwa nchini huko mwishoni mwa wiki baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kiasi cha kusababisha figo zake kushindwa kufanya kazi.Katibu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Rodrick Kabangila alisema Dar es Salaam jana kwamba, hali ya Dk Ulimboka imeimarika na kuwaomba Watanzania wamuombee apone haraka.“Taarifa tulizozipata kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba, hali ya Dk Ulimboka imezidi kuimarika tofauti na alivyokwenda, figo zimeanza kufanya kazi ingawa kwa polepole na amefanyiwa vipimo vingine,” alisema Dk Kabangila na kuongeza:“Pia ameanza kuzungumza, anawatambua watu vizuri na zaidi amewaomba Watanzania wamuombee apone haraka.” |

