photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> MAKALA:DIRA YA TAIFA YAZIDI KUTOWEKA

MAKALA:DIRA YA TAIFA YAZIDI KUTOWEKA

Posted on Jul 15, 2012 | No Comments


  Na Peter uiso
          Licha ya kuonekana na umbo dogo vilevile ni kijana anaye jituma na kuudhirishia umma wa watanzani  kuwa  anayoyasema ndani na nje ya bunge ni ya kweli pasipo kuwa na kasoro Mh John john mnyika pia alisema kuwa “hapa tulipo fika ni kwa sababu ya udhaifu wa serikali yetu pomoja na mfumo wake wakiutawala”.
           Pamoja na taarifa mbalimbali zikitolewa kwa jeshi la polisi kumekuwepo na vitendo mbalimbali vya uvunjifu wa amani pasipo hatua zozote kuchukuliwa yafuatayo ni maneno ya kijana mmoja muda mfupi baada kupoteza uhai wake alisema hivi
          “Mimi ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi, Singida katika idara ya elimu. Nilishiriki katika mikutano miwili ya CHADEMA iliyofanyika Ndago na Kinampanda na nilishiriki kupokea msafara kuanzia Mbelekese. Ukweli ni kwamba utaratibu wa kuvuruga mikutano ya CHADEMA uliandaliwa mapema kwa kuwashirikisha OCD, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Iramba Magharibi, na jambo hili tuliwaeleza viongozi wa CHADEMA kabla hawajafika Ndago. Mpango uliokuwepo na utakaokuwepo katika mikutano ya leo ni kuwaandaa vijana wasio pungua 50 wakiwa wamelewa chakari. Wao kazi yao ni kuhakikisha kwamba viongozi wa CHADEMA hawahutubii mikutano na wakijifanya hawaelewi basi mawe yapopolewe. Jambo hili halijawafurahisha watumishi wengi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wanaopenda haki, na kuna malumbano makali yanaendelea chini kwa chini.

            Sasa jana, mara msafara ulipofika Ndago na kabla mkutano haujafunguliwa wale vijana walikuwa wamekaa pembe tatu tofauti nyuma ya Mnyika, mbele kabisa karibu na barabarani na kushoto wakiwa wamejichanganya na maaskari. Lengo ilikuwa ni kumlenga mawe Mnyika moja kwa moja ili ionekana kwamba hatakiwi kabisa Iramba. Bahati nzuri aliposimama Waitara akaanza na tahadhari kali sana kwamba tunafahamu mipango yote haramu na akawaambia maaskari wanawajibika kulinda mkutano kwa sababu mkutano ni halali na una baraka zote za Jeshi la Polisi. Moja ya wale vijana alimpigia simu Mwigulu kwamba mpango wao umeingia mkenge kwa sababu jamaa wa CHADEMA wanaujua mpango mzima. Mwigulu alimfokea yule kijana kwa ukali sana na akamwambia anataka kuona mawe yanapigwa ndani ya dakika tano vinginevyo ajiandae. Moja kwa moja yule kijana akawaambia wenzake kwa ishara na wakatoa mawe mfukoni wakaanza kurusha. Purukushani ziliendelea na vijana wa CHADEMA wakawa wanajihami na kuwalinda viongozi waliokuwepo kwa karibu kabisa.

            Vurugu ziliendelea kwa takribani kati ya dk 20-30, na wananchi wengi kusambaratika. Waitara na Mnyika walionekana wakiwasiliana kwa simu na kuwalaumu polisi waliokuwepo, ambao wao walikuwa wanachekacheka tu. Ndipo utulivu ukarejea na wananchi walirudi kwa kasi ya ajabu, na mkutano ukajaa tena na Mnyika akaendelea kuhutubia. Mnyika alipokuwa anamalizia hotuba yake, ndipo landrover ya FFU ikaingia ikiwa imesheheni maaskari. Mnyika akawaambia wananchi kwamba maaskari wameingia lakini baada ya fujo kutokea na wananchi wamejilinda wenyewe.


               Mkutano uliisha kwa amani, na kisha msafara ukaelekea Kinampanda palipokuwa na Mkutano mwingine. Tukiwa pale Kinampanda ndipo habari zikaanza kusambaa kwa kasi kwamba kuna kijana ameuawa. Mkutano wa Kinampanda uliisha salama na hapakuwa na kurushwa mawe. Wananchi walihudhuria kwa wingi ukizingatia pale ndipo palipo Chuo cha Ualimu cha Kinampanda”baada ya kutoa ushuuda huo kijana huyo inasemekana alipoteza uhai katika mazingira ya kutatanisha.
         Naiasa serikali kuchukua hatua kuchukua hatua mapema kudhibiti vitendo uvunjifu wa amani ambavyo vinasababishwa na wanasiasa,ili watanzania waweze kujenga imani tena na jeshi la polisi ambalo limekuwa likilaumiwa kuwakandamiza wengi wasio na hatia na kuwaacha wachache  wenye hatia.
               0713-162905

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru