photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> MWENGE WA UHURU WAWASILI JIJINI TANGA

MWENGE WA UHURU WAWASILI JIJINI TANGA

Posted on Jul 6, 2012 | No Comments

Wakimbizaji wa Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wakiwasili kwenye Viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga Mchana wa leo.Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Mh. Halima Dendegu.
Mwenge wa Uhuru Ukiwekwa katika sehemu yake Katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga ambako pia kunafanyika Tamasha la Wazi la Filamu nchini.Mwenge huo umefika uwanjani hapo kwa Kulipa Baraka Tamasha hilo ambalo linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake kisicho na Kilevi cha Grand Malt.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Cpt. Honest Mwanossa (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Tanga ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Halima Dendegu wakisikiliza kwa makini salamu na utambulisho uliokuwa ukitolewa na Mratibu wa Mbio za Mwenge Mkoa wa Tanga.
Mratibu wa Mbio za Mwenge Mkoa wa Tanga akitoa salamu na utambulisho kwa vikundi mbali mbali vilivyokuwa vikionyesha biashara zao katika Tamasha la wazi la Filamu Tanzania kwenye viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga leo.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru