photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo

Home > August 2012

August 2012

HUYU NDIYE MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA DAR-ES-SALAAM

Aug 31, 2012 Category : 1

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya wananfunzi wa vyuo vya elimu ya Juu nchini CCM, mkoa wa Dar es salaam Ndugu Asenga Damian Abuubakar, akibebwa juu juu na wapambe wake, baada ya kushinda nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa akiwakilisha wilaya ya Ifakara. Kijana huyo ambaye ni kada mkubwa wa Chama anawakilisha kundi kubwa la vijana wenye ari, uwezo na nia ya dhati ya kukisimamia Chama Cha Mapinduzi na kukiongezea nguvu na fikra mpya za Vijana ili kukijenga zaidi na kukiongezea ustawi.

HABARI ZILIZOSAMBAA ZIKIDAI BI. KIDUDE AMEFARIKI DUNIA SI ZA KWELI.

Category : 0

Habari zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii kuwa mkongwe wa muziki wa jadi visiwani Zanzibar Bi. Kidude amefariki dunia si za kweli JamiiPress imezungumza na watu wa karibu ambao wamesema kwamba Bi. Kidude bado anavuta pumzi na amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal iliyopo visiwani humo.

NEW YORK FASHION WEEK.

Category : 0


NEW YORK FASHION WEEK 
PRAJJE 1983 Spring/Summer 2013 Collection 
September 12, 2012.
CASTING DETAILS: 
WHEN: Sunday, September 2nd, 2012 
TIME: 5:00PM to 7:00PM 
WHERE: I Ella.com Studio-401 Broadway, Suite 700, New York, NY
REQUIREMENTS:
Female: 5’09” and taller, size 0-4
All models must have runway experience
Composite cards are required
A Picture ID is required to enter the building for the casting
Female models need to bring a pair of high heels (5’in or higher)
ALL MODELS ATTENDING THE CASTING MUST RSVP BEFORE CASTING DAY.
E-mail: 83.model@prajje1983.com

WANAFUNZI 51 UDSM WAACHIWA HURU

Category : 0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imewaachia huru wanafunzi 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, waliokuwa wakikabiliwa na  mashtaka ya kufanya mkusanyiko usio halali na kukaidi amri halali ya askari wa Jeshi la Polisi iliyowataka watawanyike.

Akiwaachia huru wanafunzi hao jana, Hakimu Mkazi  Waliarwande Lema alisema anawaachia huru washtakiwa hao, kwa mujibu wa kifungu cha 225 (5) cha Sheria ya  Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA), sura ya 20 kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuliendesha shtaka hilo.

Wanafunzi hao  waliachiwa huru baada ya Wakili wa Serikali, Prosper Mwangamila kudai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya  kusikilizwa na kubainisha kuwa mahakama ilikwisha toa ahirisho la mwisho Agosti 13, mwaka huu.
Mwangamila alidai kuwa waliwasiliana na mashahidi wao ambao ni askari kupitia kwa RCO wa Wilaya ya Kinondoni ,lakini aliwaambiwa  kuwa askari hao ni moja kati ya askari waliopo kwenye Sensa ambayo ni muhimu kama kesi hiyo.
Hivyo  Wakili huyo wa Serikali aliiomba mahakama itoe ahirisho lingine la mwisho  hadi Jumatatu  kwa sababu  askari hao bado  wapo kwenye Sensa ambayo inaisha Jumapili.

Baada ya kutolewa kwa hoja hizo, Wakili wa Utetezi, Regnal Martin alipinga ombi la kuahirishwa kwa kesi hiyo na kuutaka upande wa mashtaka  kuheshimu  amri ya mahakama.

Wakili Martin alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo imekuwa ikiahirishwa  kwa sababu tofauti  ikiwemo ya askari hao kuwepo kwenye mgomo wa madaktari wa Julai 12, mwaka huu.

Akitoa uamuzi juu ya hoja hizo, Hakimu Lema alisema baada ya kupitia mwenendo mzima wa kesi , mahakama inajiuliza  swali  kuwa mashahidi pekee ni hao hao maaskari na kama ni hao  upande wa mashtaka ulipaswa kuwasilisha hati chini ya kifungu cha sheria cha 225 (4) cha CPA ambacho kinaeleza tarabu kama shahidi hayupo nini kifuatwe.
Hakimu Lema alisema sababu zilizotolewa na upande wa mashtaka ni  za msingi lakini hazikubaliki  na kwamba walichokifanya wameidharau mahakama kwa kutofuata taratibu zilizopo.

Aliongeza kuw ana wasiwasi  hata kutoa ahirisho lingine la mwisho kwa upande wa mashtaka  kwa sababu akitoa ahirisho hadi Jumatatu wanaweza kwenda na sababu nyingine kuwa askari hao wapo kwenye matukio yaliyotokea baada ya Sensa.

Baada ya kuangalia  mwenendo mzima wa kesi hiyo, Hakimu aliliondoa shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 225 (5) sura ya 20  kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuliendesha shtaka hilo.

Wanafunzi  walioachiwa huru ni Mwambapa Elias,Evalist Elias, Baraka Monesi, Hellen Mushi, Alphonce Lusako, Matrona Babu, Rolana Wilfred, Godfrey Deogratius , Munisi Denis,Evanos Gumbi pamoja na wenzao 40.

Awali Wakili wa Serikali, Ladslaus  Komanya alidai kuwa mnamo Novemba 11 mwaka huu,  eneo la Mlimani la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja walifanya mkusanyiko usio halali na kusababisha uvunjifu wa amani  eneo hilo.

Komanya alidai kuwa  washtakiwa hao wakiwa kwenye mkusanyiko huo haramu kwa lengo la kufanya mgomo, askari wa Jeshi la Polisi waliwataka watawanyike, lakini hata hivyo wanafunzi hao walikaidi amri hiyo na kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hata hivyo washtakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, walikana mashtaka hayo na waliachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika ambaye alisaini bondi ya Sh1milioni.

VOTE FOR THE SERENGETI MIGRATION AS ONE OF WOUNDERS OF THE WORLD.

Category : 0

The great migration, taking place twice in a year, once when they leave and again when they return home, is an extraordinary scene! And because of this Serengeti Migration gets a nominee for Seven Natural Wonders Of Africa. Send your votes to vote@sevennaturalwonders.org, putting Tanzania in the subject field and ranking your top 7 from http://sevennaturalwonders.org/category/africa/

BEST INTERIOR DESIGNS OF THE DAY..

Category : 0



FAKE CAR ENGINE OIL FLOODS THE MARKET IN UGANDA

Category : 0

 Police and UNBS officials display some of the oil drums that were found  in Hajj Shafik Lukyamuzi’s House in Bulenga on Wednesday.
Police and UNBS officials display some of the oil drums that were found in Hajj Shafik Lukyamuzi’s House in Bulenga on Wednesday. 

Counting losses: The most affected products are Total lubricants, particularly Total Lubia Oil 6200 for which the packaging has been copied.

NAFASI 6 ZA KAZI TANESCO TANZANIA.

Category : 16

Procurement Officer
TANESCO

Date Listed: Aug 31, 2012
Phone: No Calls Please
Area: Dar Es Salaam
Application Deadline: Sep 13, 2012

Position Description:
TTS -City Centre Ref.No.02
The successful candidate will be responsible for implementation of procurement processes (goods, works and services) in a transparent, objective, economic and efficient manner, consistent with relevant policies, legislation, regulations and guidelines in accordance to Public Procurement Act, 2004 and any other International procurement guidelines.
Minimum Requirements;
A good bachelor degree in Procurement / BBA in Procurement and Supplies Management
BBA in Procurement and Logistics Management or its equivalent in the field
CPSP will be an added advantage.
At least 2 years of working experience
Must be Computer literate
Other Attributes for All Positions
The ability to learn fast and adapt to change easily, and have the ability to work under pressure and tight deadlines
Remuneration
An attractive compensation package base on performance and consummate with the responsibility will apply to the successful candidates. All positions with terms of employment are performance based on fixed contract.


Supplies Officer (2 Posts)
TANESCO

Date Listed: Aug 31, 2012
Phone: No Calls Please
Area: Dar Es Salaam
Application Deadline: Sep 13, 2012

Position Description:
TTS - City Centre Ref. No. 05
Successful candidates will be responsible for managing supplies activities including control stocks and issues materials to ensure efficient delivery, and manage transport fleet for smooth operation. He/ she will also play role of advising Senior Transport and Supplies Officer regarding supplies matters to ensure adherence to the Public Procurement/ Supplies regulations.
Minimum Requirements;
A good bachelor degree in Materials Management / BBA in Procurement and Supplies
Management, or its equivalent in the field
At least 2 years of working experience
CPSP will be an added advantage
Other Attributes for All Positions
The ability to learn fast and adapt to change easily, and have the ability to work under pressure and tight deadlines
Remuneration
An attractive compensation package base on performance and consummate with the responsibility will apply to the successful candidates. All positions with terms of employment are performance based on fixed contract.


Receptionist
TANESCO

Date Listed: Aug 31, 2012
Phone: No Calls Please
Area: Dar Es Salaam
Application Deadline: Sep 13, 2012

Position Description:
TTS - City Centre Ref. No. 04
In this position, the successful candidate will be expected to provide good customer care, answering a multi-line switchboard quickly (ideally within 3 ring cycles) and directing calls to their destination without delay and maintain Log information on calls received, detailed and accurate records.
Minimum Requirements;
Form 4jFornl 6 Leaver
Good customer care skills
Experience of not less than 3 years in customer services field
Must be Computer literate
Other Attributes for All Positions
The ability to learn fast and adapt to change easily, and have the ability to work under pressure and tight deadlines
Remuneration
An attractive compensation package base on performance and consummate with the responsibility will apply to the successful candidates. All positions with terms of employment are performance based on fixed contract

TAASISI TA MED INTERNATIONAL YA MAREKANI KUISAIDIA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR KUFIKIA KIWANGO KINACHOKUBALIKA KITEKNOLOJIA.

Category : 0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Taasisi inayoshughulikia Taaluma ya Teknolojia ya Afya ya chuo Kikuu cha Brown Mjini Boston Nchini Marekani (Med Inaternationala ) Bw. Jayson Marwaha Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Katikati ni Mkurugenzi mwenza wa Taasisi hiyo Bw. Han Shen Chia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia Ripoti ya Uchunguzi wa Afya uliofanywa katika Hospitali za Zanzibar iliyowasilishwa na Mkurugenzi mwenza wa Taasisi ya Med International ya Nchini Marekani Bw. Han Shen Chia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Med International ya Nchini Marekani mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa Afya katika Hospitali za Zanzibar.
Mwakilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Med International ya Nchini Marekani Bw. Jayson Marwaha akielezea uchunguzi uliofanywa na Taasisi yake kwa kushirikiana na Watendaji wa Sekta ya Afya ya Zanzibar.
Taasisi inayoshughulikia Taaluma ya Teknolojia ya Afya ya chuo Kikuu cha Brown Mjini Boston Nchini Marekani (Med International) imelenga kuisaidia Zanzibar katika Sekta ya Afya ili kufikia kiwango kinachokubalika  Kiteknolojia.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mwenza wa Taasisi hiyo Bw. Han Shen Chia wakati akikabidhi Ripoti ya utafiti wa Afya uliofanywa na Wataalamu wa Taasisi hiyo katika Hospitali za Unguja na Pemba.
Bw. Han Shen akiwa pamoja na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Med International  Bw. Jayson Marwaha amesema utafiti huo uliochukuwa takriban wiki 10 umejaribu kutoa hali halisi ya mapungufu na maeneo ambayo Taasisi yao inaweza kusaidia kitaaluma  na hata uwezeshaji.
Amesema Mipango inaendelea kuimarishwa ili kuona Taasisi hiyo inawatumia Wataalamu wa Sekta hiyo kuja kutoa mafunzo kwa Walimu wa Afya Zanzibar.
Bw. Han amefahamisha kwamba utaratibu wa kuwapata wataalamu hao hasa wakati wa kipindi cha joto ambacho wanakuwa mapumziko utazingatiwa zaidi.
Kwa upande wake Mwakilishi na Mkurugenzi wa Med International Bw. Jayson Marwaha amemueleza Balozi Seif kwamba utafiti wao kwa kuanzia utaangalia zaidi kuimarisha Hospitali za Mnazi Mmoja Unguja na ya Chake Chake Pemba.
Bw. Marwaha amesema mpango huo utafuatiwa pia na Taasisi za Nchi hiyo kuweka vitega uchumi vyao vya Sekta ya Afya hapo baadaye katika Visiwa vya Zanzibar.
Amefahamisha kwamba uwekezaji huo utazingatia na kutegemea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakavyoridhia mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti hiyo.
Akitoa shukrani zake kwa hatua za Uongozi wa Taasisi hiyo ya Med Inaternational katika kusaidia sekta ya Afya Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema juhudi za Taasisi hiyo zimeanza kuonyesha mwanga wa matumaini katika sekta hiyo muhimu kwa Jamii.

ATLETICO MADRID MABINGWA WAPYA UEFA SUPER CUP, ANGALIA MATUKIO YA MECHI HIYO HAPA..

Category : 0

Chelsea suffered UEFA Super Cup humiliation as Radamel Falcao showed them what might have been with a devastating hat-trick to help hand Atletico Madrid a crushing win.
The Blues looked anything but European champions in what was one of their most clueless performances since Roman Abramovich first began his quest for the greatest prize in club football.
The Russian also spent £80million this summer in a bid to ensure he would not have to wait another eight years for more Champions League glory.
Party time: Atletico Madrid's players celebrate with the trophy at the end of the UEFA Super Cup
Party time: Atletico Madrid's players celebrate with the trophy at the end of the UEFA Super Cup

HUU NDIO UKURASA FACEBOOK UNAOUZA WANA CHUO..

Category : 1

'Campus Divas For Rich Men’ 
  
Jane 18 has just finished high school and will be joining UoN she wants a rich dude who is willing to pay her half % school fees 
“Sisi madiva tuna gharama, NYWELE, zinataka dawa! MASIKIO yanataka,hereni!! MACHO yanataka wanja na shadow! PUA inatka kipini! MDOMO, unatka lipstic! USO unataka poda na foundation! SHINGO inataka cheni! MATITI yanataka sidiria! MIKONO inataka Bangali! VIDOLE vinataka, Pete! KIUNO kinataka shanga. MA***KO yanataka chupi MIGUU inataka hina rangi na viatu. KAMA HUNA MKWANJA POLEEEEEEE,” ni baadhi ya status zinazosomeka kwenye ukurasa uitwao 'Campus Divas For Rich Men’.
Ni ukurasa maarufu sana kwenye Facebook sasa hivi nchini Kenya, ukiwa na likes 34,339. 
Ukurasa huu huonesha picha za wasichana ‘wanaodaiwa kuwa ni wanachuo’ wakijiuza na kutafuta wanaume wenye fedha ili wawatimizie haja zao.
Hata hivyo kwa uchunguzi uliofanywa na gazeti la Daily Post, umegundua mtu aliyeufungua ukurasa huo ambao kiukweli picha na majina anayoyaweka sio vya kweli.
Huyu ndiye aliyeanzisha ukurasa huo
Mtu huyo ni mvulana ambaye inasemekana kuwa alikuwa akimpenda msichana aitwaye Samira Osman lakini alipokataliwa, aliamua kufungua ukurasa huo kwa hasira.
Hivi ndivyo anavyoweka picha za wasichana zikiwa na maelezo kuwa wanataka wanaume matajiri huku maelezo akiyaandika mwenyewe.
 
Candy 20 Kenyatta university wants a rich man who can cater for her needs

WACHIMBA MIGODI 270 AFRIKA KUSINI WASHITAKIWA KWA MAUAJI YA WENZAO

Category : 0

Polisi Afrika Kusini wakipambana na wachimba migodi
Waziri wa sheria wa Afrika Kusini ametaka ufafanuzi zaidi kuhusu wachimba migodi 270, walioshtakiwa kwa kosa la mauaji ya wachimba migodi wenzao waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Waziri Jeff Radebe alisema kuwa uamuzi wa kuwafungulia mashtaka wachimba migodi hao, uliwashtua wengi na kusababisha wasiwasi miongoni mwa watu nchini humo.
Inaarifiwa viongozi wa mashtaka waliwafungulia mashtaka wachimba migodi hao kwa misingi ya kanuni za kosa la kutendwa kwa nia moja ambayo ilitumika sana wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi.
Uamuzi huo tayari umekashifiwa vikali na mawakili ya kikatiba.
Katika taarifa yake, waziri Radebe, alisema kuwa kulingana na katiba , waziri wa sheria ndiye ana usemi mkubwa juu ya mamlaka ya kitaifa kuhusu mashtaka.
Alisema kuwa ameagiza kiongozi wa mamlaka hiyo kumpa maelezo kuhusu sababu za uamuzi waliouchukua.
Polisi waliwapiga risasi wachimba migodi 34 wiki mbili zilizopita wakati wa mgomo wao katika mgodi wa madini ya Paltinum wa Marikana , unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin, ambayo ni ya tatu kwa ukubwa wa uzalishaji wa madini hayo.
Mgomo wa wachimba migodi
Watu wengi walighadhabishwa na mauaji hayo.
Hata hivyo polisi walitetea hatua yao wakisema walilazimika kuwafyatulia risasi wachimba migodi hao, walipokuwa wanakabiliana nao wakiwa wamejihami kwa mapanga.
Sita kati ya wachimba migodi hao 270 waliokamatwa na polisi wangali hospitalini wakiuguza majeraha yao.
Walifunguliwa mashtaka siku ya Alhamisi baada ya viongozi wa mashtaka kusema kuwa walikuwa miongoni mwa kundi la watu ambao vitendo vyao vilisababisha polisi kuwafyatulia risasi.

KIBONZO CHA SIKU.

Category : 0


UJUE UMUHIMU SHANGA KIUNONI KATIKA MAPENZI!...

Category : 5


Shanga ni topic tata sana kwangu kwa vile sina uzoefu nayo na kila ninapojaribu kuuliza watumiaji au wavaa huwa hawanipi majibu mazuri na yakuridhisha. Wanaume watakuambia wanapenda tu na wanawake watasema wanaume au wapenzi wao wanapenda wao wazivae.

Rafiki yangu wa Kighana alitoa maelezo ambayo nadhani yalikamilika japo hakugusua umuhimu wake kwenye ngono….aliniambia kuwa huko kwao Shanga ni muhimu kuonyesha kuwa wewe ni mwanamke wa shoka au uliyekamilika.

Ikiwa mwanamke huvai Shanga basi unaonekana hufai na hakuna mwanaume atataka kutoka na wewe/kuchumbia only kwa vile huna shanga kiuoni……hivyo wanawake wote wa Kighana wanavaa shanga no matter how beautiful, educated au westnized they are.

Turudi Nyumbani……nakumbuka niliwahi kumuuliza mama yangu (wao wanavaa shanga) faida ya shanga na yeye akanijibu kuwa ni kama sehemu ya “romance”….nikauliza ni sawa sawa na kubusu au kushikana?

Akajibu “ndio”…..nikauliza inawezekanaje mtu asisimke kutokana na kuziona shanga tu au kuzishika-shika tu? Akanijibu kuwa “mwanaume anapozichezea humpa mwanake mtekenyo furani ambao hufamfanya ajisikie raha na hamu ya kungonoka (nyege) huanza kumpanda”.

Mimi kama Dinah nikahisi kuwa mwanaume anaetegemea kuchezea shanga ili mwanamke “anyegeke” atakuwa hana utundu wa kutosha wa kutumia mikono na vidole vyake ktk kuuchezea mwili wa mwanamke hasa ukizingatia kuwa mwanamke “hanyegeki” kwakuchezewa na vidole kiunoni tu bali kona nyingi ktk mwili wake

Uvaaji wa shanga kiunoni ni moja kati ya tamaduni zetu waafrika, nakumbuka katika jamii ya Wanyamwezi (nadhani na Wasukuma pia as far as I remember miaka hiyo niliyoishi kona hizo za Tz ) shanga zilikuwa zikivishwa mtoto wa kike kiunoni na yule wa kiume alivalishwa kijikamba/uzi mweusi ambao huwa na vipande vidogo viwili au vinne vya mti akiwa mdogo.

Ssina hakika kwanini ilikuwa hivyo ila nakumbuka niliwahi kuambia kuwa vijiti vile ni kumlinda mtoto dhidi ya malaika wabaya (kama ilivyo kwa tamaduni nyingine kuwapaka watoto wanja ili watishe) na shanga ni kuonyesha kuwa mtoto ni wa kike.

Mtoto napofikia umri Fulani vikorokoro hivyo huondolewa na binti huvalishwa tena pale anapokua (vunja ungo/balehe), kule kwetu kila rangi ya shanga huwa na maana yake nikiwa na maana kama binti ni Bikira anavaa rangi Fulani, kama uliolewa ukaachika wavaa rangi Fulani, kama umeolewa wavalishwa rangi husika, kama siku hiyo wataka kufanywa (unanyege) basi wamvalia mumeo rangi husika,ikiwa ni mjamzito pia unapaswa kutuma ujumbe kwa kumvalia mumeo rangi fulani (ilikuwa mwiko kungonoka na mtoto tumboni) kama uko hedhini basi utalazimika kuongezea rangi nyekundu juu ya ile uliyonayo.

Itasaidia kama watakuja na rangi inayoashiria kuwa mtu kaukwaa a.k.a ana ngoma a.k.a UKIMWI.....wewe unaonaje?

KIBO PALACE HOTEL EVENT IT`S ON.. IT`S CORPORATE NETWORKING ON 6th SEPTEMBER.

Category : 0

WE CARE ABOUT YOUR PERSONAL SECURITY - JOIN US AT OUR CORPORATE NETWORKING EVENING ON 6TH SEPTEMBER 2012 AND LEARN MORE ON PERSONAL SECURITY

UVCCM MKOANI IRINGA WAPATA VIONGOZI WAPYA

Category : 0

 
Rais Jakaya Kikwete Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa akihutubia katika moja ya mikutano ya chama hicho.

Jumuiya ya Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM, umefanya uchaguzi na kupata viongozi wapya watakaoongoza jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mgombea ambaye amechaguliwa kuchukua nafasi ya mwenyekiti ni Bw. Kayugwa ambaye ameshinda kwa kupata kura 288 kati ya kura 463 halali zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa vijana hao.
Nafasi nyinge ambazo zimeweza kupata viongozi wapya ni pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa Bw. Deogius Kisega ambaye amepata kura 217, halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Bw. Mkenge amepita kwa kupata kura 165.
Aidha katika nafasi ya za baraza la wilaya kupitia wilaya ya Iringa vijijini Bi. Ratifa Mwasiposya amepita kwa kupata kura 392 akifuatiwa na Nuru Nkenge ambaye amepata kura 389 na Bi. Newton Mongi akiwa na kura 370.
Aidha wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa na baraza kuu la mkoa unawakilishwa na Bw. Alice Kibiki ambaye amepata kura, 233 akifuatiwa na Bw. Thomas Muyinga mwenye kura 162 kupitia wilaya ya Iringa vijijini.
Wajumbe wengine ambao wanawakilisha kwenye Baraza kuu la mkoa ni pamoja na Bw. Kanute Mhongole mwenye kura 243, akifuatiwa na Yuda Vakulule mwenye jumla ya kura 207,  na Thomas Myinga mwenye kura 199.
Viongozi hao wapya wa Jumuiya ya umoja wa vijana kupitia Chama cha Mapinduzi wamesema wanatarajia kuleta mapinduzi ya mabadiliko katika kuleta maendeleo ya vijana ikiwemo kuwawezesha vijana kujitegemea katika ajira.          

BENKI KUU YAZINDUA RASMI MFUMO WA MAWAKALA KUNUNUA DHAMANA KWA NJIA YA MTANDAO.

Category : 0

Gavana Ndullu akibonyesha kitufe cha Komputya kuashiria uzinduzi rasmi wa mfumo wa mawakala wa Benki hiyo wa kununua dhamana na hati fungani kwa njia ya mtandano (online) kwenye mnada. (Picha ma Tiganya Vincent wa Maelezo –Dar es Salaam).
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Benno Ndullu akizundua rasmi mfumo wa mawakala wa Benki hiyo wa kununua dhamana za Serikali na hati fungani kwa njia ya mtandano(online) kwenye mnada na hivyo kupunguza ule utaratibu wa dhamana wa kupeleka karatasi katika Benki ili kupata huduma hiyo.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Benno Ndullu akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mfumo wa mawakala wa Benki hiyo wa kununua dhamana za Serikali na hati fungani kwa njia ya mtandano (online) kwenye mnada na hivyo kupunguza utaratibu wa dhamana wa kupeleka karatasi katika Benki ili kupata huduma hiyo. 
Profesa Ndullu (kushoto) na Naibu Gavana wa BoT Dkt Natu Mwamba (kulia) wakinukuu maswali mbalimbali ya waandishi wa jijini Dar es salaam kabla hawajaanza kuyatolea ufafanuzi.

HUYU NDIYE MWIGIZAJI MAARUFU WA NIGERIA ALIYEMUUA MKEWE KWA SUMU

Category : 0

Rich Oganiru

Kwa watazamaji wa filamu za kinaijeria, sura ya Rich Oganiru si ngeni machoni.
Ni muigizaji maarufu wa filamu hizo na tayari ameshaigiza zaidi ya filamu 300.
Kwa mujibu wa jarida la National Enquirer la Nigeria, Oganiru anakabiliwa na kesi nzito ya mauaji ya mke wake mfanyabiashara bilionea aliyekuwa akiishi Abuja.
Huyo hakuwa mke wake wa kwanza kwani mke wake wa awali naye alikufa katika mazingira yasiyoeleweka miaka kadhaa iliyopita.
National Enquirer limedai kuwa muigizaji huyo alikuwa akiishi maisha duni kabla ya kukutana na mwanamke huyo mfanyabishara aliyebadilisha maisha yake.
Inadaiwa kuwa baada ya kifo cha mke wake aliyezaa naye watoto wawili wa kiume, alijikuta katika maisha magumu kiasi cha kukosa hata hela kununua chakula na ndipo alipokutana na mwanamke huyo aliyemwimbisha na kueleweka hasa kutokana na sura yake kuwa maarufu kwenye filamu.
Ripoti inasema kuwa baada ya kuishi pamoja na kuoana na mwanamke huyo, Rich alianza kulalamika baada ya mkewe kushindwa kushika mimba.
Inaendelea kudai kuwa mke wake alimwamini na kumfanya awe mmiliki wa baadhi ya mali zake na kuwa mwamuzi wa mambo ya kifedha kwenye kampuni yake.
Baadaye Rich aliingiwa na tamaa na kuanza kuwa na uhusiano na msichana mdogo aitwaye Iyake.
Ilikuja kugundulika kuwa mke wake anashindwa kupata mimba kwasababu alikuwa akisimbuliwa na tatizo la Fibroid.
Rich anadaiwa kumshawishi mke wake akafanyiwe upasuaji wa kuondoa tatizo naye akakubali.
Ripoti inasema mke wake alifariki muda mfupi baada ya upasuaji huo kwa madai kuwa Rich alimtembelea hospitali na kumpa kidonge bila ruhusa ya daktari kwa kudai kuwa kidonge hicho kingempunguzia maumivu bila kujua kuwa ilikuwa sumu.
Baada ya daktari kubaini kuwa mikono yake ilikuwa salama aliagiza kufanyike uchunguzi kwa mwili wa mwanamke huyo na ukabaini kuwa alipewa sumu.
Sumu hiyo ilionesha kuwekwa katika muda ambao mume wake alikuwa amekwenda kumsalimia kabla ya kufariki mke wake.
Muigizaji huyo alikuja kukiri kumuua mke wake baada ya kupokea mateso makali kutoka kwa polisi.
Hivi sasa Rich anashikiliwa kwenye kituo cha polisi mjini Abuja wakati mwili wa mke wake ukiwa mortuary.

DIAMOND NA MAMA YAKE ENZI HIZO

Category : 1

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ANATARAJIA KUHUDHURIA MAZISHI YA ASKOFU KIKOTI..

Category : 0

Na mwandishi, Bilhuda Msangi
Waziri mkuu MIZENGO PINDA  anatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa askofu wa kwanza wa kanisa katoliki jimbo la mpanda PASCHAL KIKOTI yatakoyo fanyika kesho mkoani Rukwa.

rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh.Dkt.Jakaya Mrisho kikwete amemtumia salamu za rambirambi rais wa baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu William paschal Kikoti.


Askofu kikoti alifariki jumanne ya agosti 28,2012 katika hospital yaBugando jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa shinikizo la damu.

Mwili wa marehemu umeshawasili mjini mpanda na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa dini kwa ajili ya mazishi yake kesho.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe......ameen 

HIVI NDIVYO MBUYU TWITE MCHEZAJI WA YANGA ALIVYOPOKELEWA JANA UWANJA WA NDEGE.

Category : 0

 Beki mpya wa Mabingwa wa Kombe la Kagame, Dar Young Africans, Mbuyu Twite akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana akitokea Kigali Rwanda na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa soka.
 Mchezaji nyota kutoka timu ya APR ya Rwanda Mbuyi Twite akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, baada ya Yanga kumpa mapokezi makubwa alipowasili jana kukipiga na timu hiyo.
 Mbuyu Twite akiwa amevalishwa jezi namba 4 iliyoandikwa Rage
  Moja wa mashabiki aliyekuja katika mapokezi ya Mbuyu Twite akiwa amelala chini
 Mashabiki wa Yanga.Picha zote na Mdau Francisdande, Habari na Sosthenes Nyoni

 TWITE, Twite, Twite' kiitikio 'Rage, Rage, Rage' ndiyo wimbo  uliotawala jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati beki mpya wa Yanga, Mbuyu Twite alipowasili akitokea Rwanda.

Wimbo huo ulikuwa ukiimbwa na mamia ya mashabiki wa Yanga wake kwa waume waliofurika uwanjani hapo kwa ajili ya kumpokea beki huyo.

Kwa wiki kadhaa Twite aliteka hisia za mashabiki wa timu za Yanga na Simba ambazo ni baada ya beki huyo kusajiliwa na timu hizo kabla ya yeye mwenyewe kuikana Simba na kuamua kuichezea Yanga.

Kitendo hicho, kilisababisha kuzuka kwa malumbano baina ya viongozi wa klabu hizo mbili na kufuatiwa na tamko la Makamu mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu kusema kuwa watamkamata Twite na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria  atakapokanyaga ardhi ya Tanzania.

Hata hivyo licha ya vitisho hivyo vya Kaburu, hakuna kiongozi yeyote wa Simba aliyeonekana uwanjani hapo kumsubiri beki huyo kwa ajili ya kumtia mikononi kama ilivyotarajiwa.

Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo majira ya saa10.30 jioni, Twite alipokewa na viongozi wa Yanga wakiongozwa na katibu mkuu wa timu hiyo, Selestine Mwesigwa na alikabidhiwa jezi namba 4 yenye jina la Rage  kama ushindi dhidi ya wapinzani wao Simba.

Mara baada ya kukabidhiwa jezi hiyo, Twite alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa umati aliouhushuhudia uwanjani hapo ulimpa moyo wa kuona jinsi mashabiki wa Yanga wanavyomjali.

"Nimeshangaa sana kuona watu wengi kiasi hiki, hii inadhihirisha ni kiasi gani mashabiki wananijali, nami nasema sitawaangusha, jambo la muhimu ni ushirikiano tu kutoka kwao na uongozi mzima wa Yanga ili malengo yafikiwe,"alisema Twite.

Alipoulizwa anazungumziaje mpango wa Simba kutaka kumkamata kwa madai ya kuwatapeli, Twite alisema,"kwa sasa siwezi kuzungumzia hilo, nadhani nitafanya hivyo baadaye."

Baada ya mahojiano na Wanahabari, Twite alipanda gari dogo na moja kwa moja msafara ulioongozwa na mabasi yaliyokuwa yamebeba mashabiki wa Yanga ulielekea makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko Mtaa wa Jangwani.