TAARIFA ZA MKUTANO WA CHADEMA IRINGA LEO
Posted on
Aug 28, 2012
|
1 Comment

Taarifa kutoka mkoani Morogoro zinapasha kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeamua kusitisha mkutano wake wa Mkoani Iringa hii leo na mingine yote kupisha zoezi la Sensa kitaifa kama walivyoombwa kufanya hivyo na serikali na Jeshi la Polisi. Aidha Viongozi hao wakitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari wamepasha kuwa mara baada ya zoezi la sensa Operesheni Sangara itaendelea kama kawaida na dola isije ikaleta sababu zingine za kuto wapa vibali vya kufanya mikutano yao. Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde.
Serikali siku zote imekuwa na woga na mabadiliko ya kisiasa.Serikali dhalimu siku zote duniani mwisho wake ni anguko,ccm pamoja na magamba yote sasa wako chali,Napenda kusisitiza tutaendelea na mtitimtiti huu mpaka tuingie madarakani 2015.tusirudi nyuma kwa sabbu ya mabomu wala risasi za moto ndugu zangu.hii ndiyo vita bado mbichi
ReplyDelete