HICHI NDICHO WALICHOSEMA WALIOTAKA KUMUUA ALI KIBA..
Posted on
Aug 29, 2012
|
1 Comment
![]() |
TID |
Jana kumevuma habari kuwa mwanamuziki wa Bongo Flava Khalid Mohamed aka Top In Dar, anashikiliwa na polisi baada ya kushutumiwa kuwa alipanga njama za kumuua msanii mwenzie Ali Kiba.
Leo kupitia XXL ya Clouds FM, meneja wa Ali Kiba amezungumza kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo.
![]() |
Ali Kiba |
Anasema ni kweli walipata ujumbe unaosema kuwa kuna watu waliokuwa wametumwa kwenda kumuua Ali Kiba.
"Baada sasa ya taarifa hizo kuifikia familia, iliamua kuripoti jambo hilo polisi, polisi walifika eneo lile na kulikuwa kuna watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani na pale Ali Kiba anaishi wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu kuchunguza hili na lile. Sasa baada ya watu wa karibu kuwaona na kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatlia na kuwaweka chini baada ya kuwakamata.
Walipowahoji vizuri wakasema kwamba ni kweli wao wametumwa kuja kufanya jambo hlo hapo kwa Ali Kiba na wao sio wenyeji wa Dar es Salaam wametoka mikoani. Walipoulizwa ni nani ambaye amewatuma kuja kufanya hilo jambo wakawa wamemtaja TID Kwamba moja kwa moja yeye ndo anahusika. Basi moja kwa moja gari la jeshi la polisi likaenda kumkamata TID na hatimaye kumfikisha kwenye kituo cha polisi cha kati ambapo yupo mpaka hivi sasa anashikiliwa."
labda tukijua kuwa kisa nn
ReplyDeletelakini pia mi naona kuwa nn
huo ni uboya tu sema
alikiba anamafanikio sana
so wengine ndo hawataki kuona jembe ali k
anaendelea uyo aachwe huko
aaaaaaaah tid naye