photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > OLIMPIKI YA WALEMAVU "YAREJEA NYUMBANI" UINGEREZA

OLIMPIKI YA WALEMAVU "YAREJEA NYUMBANI" UINGEREZA

Posted on Aug 30, 2012 | No Comments


 ufunguzi wa paralympics
Malkia wa Uingereza ametangaza kuanza rasmi kwa Olimpiki ya walemavu jijini London mwaka 2012, wakati wa sherehe zilizohudhuriwa na watu 80,000.
Mwanamichezo wa Uingereza aliyepata medali ya kwanza ya dhahabu ya Olimpiki ya walemavu, Margaret Maughan, 84, alipewa heshima ya kuwasha mwenge uwanjani.
Kiongozi wa mashindano hayo Lodi Coe aliwaambia waliohudhuria: " Jiandaeni kuhamasishwa, jiandaeni kufurahishwa, jiandaeni kupata burudani."
Mapema, wanamichezo walipita kwenye uwanja huo mkuu, huku wanamichezo wa Uingereza wakiwa wa mwisho kuingia uwanjani na kushangiliwa zaidi.
 
' Michezo itakumbukwa'
Sherehe za ufunguzi ziliashiria kuanza kwa mashindano hayo ya siku 11 kwa wanamichezo 4,200 kutoka nchi 164, ikiwemo wanamichezo 300 kutoka Uingereza.
Mchezo wa mpira wa kikapu kwa walemavu, kulenga shabaha, kuogelea na kuendesha baiskeli ni miongoni mwa michezo inayotarajiwa kufanyika siku ya kwanza.
Lodi Coe amewaambia waliohudhuria katika uwanja huo mashariki mwa London: " Ni furaha kubwa kwangu kusema karibuni nyumbani kwa michezo ya Olimpiki ya walemavu."
Alisema Uingereza "iko tayari" na waliohudhuria watazidisha hamasa", akiongeza: " Michezo hii itakumbukwa."
Wachezaji wanane wa timu ya mpira wa kikapu ya Uingereza walipewa heshima ya kubeba bendera ya Olimpiki ya walemavu hadi kwenye uwanja.Bendera ilipandishwa na wanajeshi, kabla ya Malkia kutangaza kufunguliwa rasmi kwa michezo hiyo.
 
Muogeleaji wa Uingereza Liz Johnson, aliyepata medali katika michezo ya Beijing 2008, muamuzi wa raga ya walemavu Richard Allcroft na David Hunter, anayefunza timu ya mchezo wa farasi, wote walikula kiapo rasmi kwa niaba ya wanamichezo na waamuzi.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru