photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > WANAJESHI WA AUSTRALIA WAUAWA AFGHANISTAN

WANAJESHI WA AUSTRALIA WAUAWA AFGHANISTAN

Posted on Aug 30, 2012 | No Comments

Wanajeshi watano wa Australi wameuawa nchini Afghanistan katika mashambulizi mawili mabaya.
Wanajeshi wengine watatu waliuawa na mtu aliyekuwa amevalia magwanda ya jeshi katika eneo la Uruzgan siku ya jumatano. Haya ndio mashambulizi ya hivi karibuni katika kile kinachotajwa kuwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa dhidi ya wanajeshi wa Australia.
Katika tukio jingine,wanajeshi wengine wawili waliuawa katika ajali ya helikopta mkoani Helmand mapema leo.
Waziri mkuu wa Australia Julia Gillard amenukuliwa akisema kuwa katika vita vyenye hasara kubwa, hii ndio siku mbaya zaidi kwa wanajeshi wetu nchini Afghanistan.
Bi Gillard ameondoka visiwani Cook, ambako alikuwa anahudhuria mkutano mkutano wa viongozi wa visiwa vya Pacific kuerejea nchini Australia.
"Baada ya kupokea habari hizi nimeamua ni muhimu kwangu kurejea nyumbani' alisema bi Gillard.
Waziri wa muda wa ulinzi, bwana Binsikin, alisema kuwa familia za wanajeshi hao tayari zimepashwa habari.
"Australia imepoteza wanajeshi wake watano hii leo. Ni wanajeshi waliojitolea kuhudumia nchi yetu'' alisema waziri Binskin.
Tayari mwanaume mmoja anayeshukiwa kuhusika na mashambulizi hayo anasakwa na maafisa wa ulinzi wa kimataifa.
Bwana Binskin alisema kuwa mwanaume huyo aliwafyatulia risasi na kuwaua wanajeshi watatu wakati walipokuwa wanapumzika na kuwajeruhi vibaya wengine wawili.
Alisema kuwa wanajeshi hao watatu wenye umri wa miaka 40, 23 na 21, walikuwa katika kambi ya jeshi eneo la Gallipoli huko Brisbane.
Takriban wanajeshi 1,500 wa Australia wanashika doria katika mkoa wa Uruzgan

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru