TAARIFA KWA UMMA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA
                              Posted on 
                              Aug 11, 2012
                            |
                            
                                  No Comments
                                  
Katika  Gazeti la Business Times toleo nambari 1248 la Ijumaa, tarehe 10 Agosti  2012, ziliandikwa habari zenye kichwa cha habari chenye maana kuwa  “Operesheni za NBC zawekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu”. Katika  habari hiyo ilielezwa kuwa Benki Kuu imechukua hatua hiyo kufuatia  ripoti za tuhuma kadhaa zihusuzo udhaifu katika uendeshaji wa benki na  utawala bora.
Benki  Kuu inapenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa haijaweka  operesheni/shughuli za NBC chini yake. Benki hiyo inajiendesha yenyewe  kwa kufuata utaratibu wa Sheria za Makampuni, 2002, Sheria ya Mabenki na  Taasisi za Fedha 2006 na miongozo itolewayo na Benki Kuu kama zilivyo  benki zingine. Wateja wa NBC na Umma kwa ujumla wanashauriwa kuendelea  kufanya biashara na benki hii kama kawaida.
IMETOLEWA NA BENKI KUU YA TANZANIA 
11AUGUST 2012
 
 
 
 

 
 
 
 
