photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 KATIKA PICHA MKOANI TANGA

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 KATIKA PICHA MKOANI TANGA

Posted on Aug 27, 2012 | No Comments

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego pichani kati mwenye kipaza sauti akisoma namba za washindi waliojinyakulia piki piki mbili zilizotolewa na kampuni ya Push Mobile,wa tatu kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rugambo Rodney na mwisho kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga,na nyuma kabisa ni Mkurugenzi wa utafiti Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Ephrahim Mafuru wakishuhudia tukio hilo kwenye uwanja wa Mkwakwani ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lililofanyika.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga mara baada ya kuwataja washindi waliojishindia piki piki mara baada ya kuchezeshwa bahati nasibu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea,pichani kati ni Afisa Mahusiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga.
Msanii kutoka THT,ajae kwa kasi katika anga ya muziki wa bongofleva aitwaye Rachel akiimba jukwaani.
Nuru akiimba kwa manjonjo na shabiki wake jukwaani.
 

Pichani shoto ni Mkurugenzi wa Masoko,Ephrahim Mafuru,Mkuu wa Vipindi Clouds FM,Sebastian Maganga sambamba na Meneja wa bia ya Serengeti,Allan Chonjo wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kurindima.
Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua ngoma 
Sehemu ya umati wa wakazi wa Tanga wakifuatilia kwa makini makamuzi ya Fiesta.


Moja ya zao la Supa Nyota kutoka Mkoani Mbeya akiimba jukwaani.
Hapatoshi Tanga usiku huu.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru