UZINDUZI WA MRADI WA TOA TAARIFA UWE SALAMA BARABARANI JIJINI MWANZA
Posted on
Aug 27, 2012
|
No Comments

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani ,Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP ) Mohamed Mpinga wa kwanza kulia, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza ,Kamishna Msaidizi (ACP) Liberatus Barlow ( wa pili kutoka kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi mwenye suti,wakiwa wameshika bango lenye namba za kudumu za Makamanda wa vikosi vya Usalama barabarani wa mikoa ya Kanda ya ziwa, zitakazotumika kutoa taarifa kwa jeshi hilo ,kuhusu ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani unaofanywa na madereva wa magari ya abiria.Katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika kituo kikuu cha mabasi Nyegezi na kuhudhuriwa na maofisa wa jeshi la polisi

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani, SACP Mohamed Mpinga akiwaelekeza abiria jinsi ya kutumia namba za kamanda wa vikosi vya usalama barabara,wakati madereva wanapokiuka kanuni na sheria za usalama barabarani wawapo safarini .Abiria wanapaswa kutoa taarifa kupitia namba hizo za simu ambao zitakuwa hewani kwa saa 24.Mpinga alikuwa akizindua mradi wa Toa taarifa Uwe salama unaofadhiliwa na Benki ya posta nchini kwa shilingi milioni 30.

Kamanda Barlow akielekeza jambo namna ya kutumia namba za kudumu za RTO wa mikoa yan kanda ya Ziwa zilizopo kwenye bango lililobandikwa ndai ya basi la abiria katika kituo cha mabasi Nyegezi muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa Toa Taarifa uwe Salama,mradi unaofadhiliwa na Benki ya Posta Tanzania kwa ajili ya kupunguza na kutokomeza ajali za barabarani nchini.